Marjaa Dini mkuu aitaka serikali iwachukulie hatua watu walio fanya jinai kwa waandamanaji au askari na raia

Maoni katika picha
Marjaa Dini mkuu ameitaka serikali ya Iraq imchukulie hatua kila aliyeshiriki katika jinai ya kuuwa au kujeruhi au kufanya shambulio lolote kwa waandamanaji au vyombo vya ulinzi na usalama.

Ameyasema hayo siku ya Jumapili mwezi (24 Muharam 1442h) sawa na tarehe (13 Septemba 2020m) alipokutana na Jenin Haines, muwakilishi maalum wa katibu mkuu wa umoja wa mataifa hapa Iraq, lifuatalo ni tamko kuhusu swala hilo:

Tunaiomba serikali imchukulia hatua kila aliyeshiriki katika jinai ya kuuwa au kujeruhi au kufanya shambulio lolote kwa waandamanaji au vyombo vya ulinzi na usalama, au aliharibu mali za umma au binafsi, tangu lilipo anza vuguvugu la kudai mabadiliko (islahi) mwaka jana, hususan wale waliofanya vitendo vya utekaji na mashambulio mengine.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: