Marjaa Dini mkuu: Kuwachukulia hatua watu waliofanya makosa ya jinai kwa waandamanaji na askari ni jambo linalotakiwa kufanyika siku yeyote.

Maoni katika picha
Marjaa Dini mkuu amesisitiza kuwa; inatakiwa kumchukulia hatua kila aliyeshiriki katika jinai ya kuuwa au kujeruhi au kufanya shambulio lolote kwa waandamanaji au vyombo vya ulinzi na usalama, au aliharibu mali za umma au binafsi, tangu lilipo anza vuguvugu la kudai mabadiliko (islahi) mwaka jana, hususan wale waliofanya vitendo vya utekaji na mashambulio mengine.

Ameyasema hayo siku ya Jumapili mwezi (24 Muharam 1442h) sawa na tarehe (13 Septemba 2020m) alipokutana na Jenin Haines, muwakilishi maalum wa katibu mkuu wa umoja wa mataifa hapa Iraq, lifuatalo ni tamko kuhusu swala hilo:

Hakika kuwachukulia hatua watu waliofanya makosa tuliyo taja ni jambo linalotakiwa kufanyika siku yeyote, ni njia sahihi ya kuzuwia jambo hilo lisirudiwe tena na kuogopesha watu wengine kufanya hivyo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: