Marjaa Dini mkuu: Kulinda heshima ya taifa kunahitaji msimamo wa kizalendo katika maswala mbalimbali yanayo gusa maslahi ya Iraq kwa sasa na baadae

Maoni katika picha
Marjaa Dini mkuu amesisitiza kuwa; Kulinda heshima ya taifa na kuzuwia kuingiliwa na ushawishi wa kutoka nje ya taifa katika mambo ya ndani ya nchi na kuzuwia mpasuko wa taifa ni jukumu la kila mtu, ni jambo la kizalendo na kulinda maslahi ya wairaq sasa na baadae.

Ameyasema hayo siku ya Jumapili mwezi (24 Muharam 1442h) sawa na tarehe (13 Septemba 2020m) alipokutana na Jenin Haines, muwakilishi maalum wa katibu mkuu wa umoja wa mataifa hapa Iraq, lifuatalo ni tamko kuhusu swala hilo:

Kulinda heshima ya taifa na kuzuwia kuingiliwa na ushawishi wa kutoka nje ya taifa katika mambo ya ndani ya nchi na kuzuwia mpasuko wa taifa ni jukumu la kila mtu, ni jambo la kizalendo na kulinda maslahi ya wairaq sasa na baadae, jambo hilo haliwezi kufanikiwa kama watu wataweka mbele maslahi binafsi, ya chama au eneo, ni jukumu la kila mtu kuweka mbele maslahi ya taifa na kujiepusha na jambo lolote linaloweza kuvunja amani na utulivu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: