Maahadi ya Quráni tukufu imemaliza mzunguko wa kwanza wa mashindano ya (Fedha) yanayo endeshwa kwa njia ya mtandao

Maoni katika picha
Wanafunzi sabini (70) wa Maahadi ya Quráni tawi la wanawake chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu, wamemaliza mzunguko wa kwanza wa mashindano ya kuhifadhi Quráni (Fedha) yanayo endeshwa kwa njia ya mtandao (Goole Meet), kwa sababu ya kuwepo kwa maambukizi ya virusi vya Korona na kuheshimu maelekezo ya idara ya afya na muongozo wa Marjaa Dini mkuu ya kujiepusha na misongamano.

Kwa mujibu wa maelezo ya kiongozi wa Maahadi bibi Manaal Jaburiy, amesema: “Hakika shindano la kuhifadhi Quráni tukufu hufanywa kila mwaka na wanafunzi wa Maahadi yetu, tumesha toa wanafunzi walio shiriki kwenye mashindano makubwa ya kitaifa na kimataifa na wakapata nafasi za juu, washiriki huwekwa katika makundi tofauti kutokana na majuzuu waliyo hifadhi pamoja na uwezo wao, mashindano waya yalikuwa ya juzuu tano na kumi kwa washiriki wenye umri tofauti”.

Kumbuka kuwa shindano la (Fedha) la kuhifadhi Quráni tukufu tawi la wanawake hufanywa kila mwaka na washiriki wakike peke yake, kwa lengo la kujenga moyo wa ushindani katika kuhifadhi Quráni tukufu, mwaka huu shindano hili limefanywa kwa njia ya mtandao kutokana na kuwepo maambukizi ya virusi vya Korona, hivyo Maahadi imelazimika kuendeleza ratiba za masomo yake pamoja na mashindano ya kuhifadhi Quráni kwa njia ya masafa (mtandao).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: