Mahudhurio makubwa katika Atabatu Abbasiyya tukufu kwenye maonyesho ya kimataifa ya vitabu (Taratiilu Sajjaadiyyah)

Maoni katika picha
Kutokana na rekodi za ushiriki wake wa kwanza na kuendeleza mwenendo wa kusambaza elimu na utamaduni wa Ahlulbait (a.s) na kila linalochangia kuboresha utamaduni wa watu, Atabatu Abbasiyya tukufu kama kawaida yake kila inapo shiriki, imepata muitikio mkubwa katika maonyesho hayo ya kimataifa (Taratiilu Sajjaadiyyah) awamu ya saba, yanayo simamiwa na Atabatu Husseiniyya tukufu katika eneo la uwanja wa katikati ya haram mbili takatifu, yamefunguliwa leo siku ya Jumatatu mwezi (25 Muharam 1442h) sawa na tarehe (14 Septemba 2020m) na yataendelea kwa muda wa siku kumi.

Rais wa kitengo cha elimu na utamaduni Dokta Sarhani Jaffaat amesema kuwa: “Tumeshiriki kupitia vitu vinavyo onyeshwa na matawi ya Atabatu Abbasiyya tukufu, ambayo ni kitengo cha elimu na utamaduni, kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu, kupitia machapisho na matoleo yao, na kazi za uandishi zilizo fanywa na wataalamu wa vitengo hivyo, wameshiriki bega kwa bega na taasisi zingine za usambazaji kwenye maonyesho hayo”.

Akaongeza kuwa: “Tawi la elimu na utamaduni limesheheni vitu vya aina mbalimbali, kama vile vitabu, cd tofauti za kidini, Akhlaq, Tarbiyya pamoja na za sekula, na vitabu vilivyo fanyiwa uhakiki na kuandikwa katika sura mpya, machapisho hayo yanawagusa watu wa rika zote, nalo tawi la kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu, linamachapisho mbalimbali ya kitengo hicho na vituo vilivyo chini yake pamoja na machapisho kuhusu masomo ya Quráni yanayo tolewa na Maahadi ya Quráni tukufu”.

Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu imesha shiriki mara ngini katika maonyesho mbalimbali ya kimataifa, yanayo lenga kusambaza fikra ya uislamu halisi na kumuwezesha msomaji kupata vitabu tofauti vya fani mbalimbali.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: