Kuanza sehemu ya pili ya program ya katuni za Alkafeel za kielektronik

Maoni katika picha
Kituo cha utamaduni wa familia chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kimetangaza kuanza hatua ya pili ya program ya kitamaduni na kimalezi, baada ya hatua ya kwanza kukubalika na kupata mwitikio mkubwa.

Mkuu wa kituo hicho bibi Asmahani Ibrahim ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Ili kunufaika na matukio ya kidini na kuyafanya yajulikane vizuri, likiwepo tukio la Ashura, kitengo chetu kumeamua kuendesha program maalum kuhusu kitio hilo, kwa namna ambayo inaendana na watoto wenye umri mdogo pamoja na uwelewa wao, aidha tumeandaa zawadi kwa watakaoshinda ili kuwapa moyo zaidi wa kushiriki”.

Akaongeza kuwa: “Awamu hii tunalenga mambo yafuatayo:

  • 1- Kutumia muda wa faragha wa watoto kwa mambo yenye manufaa kwao kiroho kuhusu tukio la Twafu la Husseiniyya.
  • 2- Kufundisha na kushajihisha watoto kuwa na mwenendo mzuri pamoja na kutambua historia ya Ashura”.

Masharti ya kushiriki ni:

  • 1- Program hii ni ya watoto wa kiume na wakike wenye umri wa miaka sita (6) na wasiozidi miaka (11)
  • 2- Program itaanza siku ya Jumamosi (12 Septemba 2020m) hadi (22 Septemba 2020m).
  • 3- Kazi zitumwe kwenye link ya Telegram ifuatayo: https://t.me/Thaqafaasria pamoja na kutaja umri wa mshiriki, mkoa anaoishi na namba ya simu ya mzazi au mlezi wake, kazi itakayo kosa vitu vivyo haitapokelewa, ili kushiriki fungua link ifuatayo: https://forms.gle/Ccs8f4jEWYGkDH7n7”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: