Akaongeza kuwa: “Tulianza mapema kujiandaa kwa ajili ya ziara hii, maandalizi yamehusisha vitu vingi, miongoni mwa vitu hivyo ni:
- - Kuandaa kumbi maalum za kupokelea mazuwaru.
- - Kupuliza dawa za kujikinga na maambukizi kwenye majengo.
- - Kuandaa jiko na kuweka aina zote za chakula kinacho hitajika.
- - Kufanya ukarabati vifaa vya umeme.
- - Kufanya ukarabati wa vyoo na kuweka mahitaji yote muhimu na vifaa vya usafi.
- - Kuandaa mabango ya vituo vya afya kwa kushirikiana na idara ya afya ya mkoa wa Karbala upande wa wanaume na wanawake.
- - Kuandaa sehemu maalum za kusaidia watu waliopotea au kupotelewa.
- - Kuweka utaratibu wa kutoa maelekezo kwa mazuwaru chini ya muongozo wa idara ya afya.
- - Kuandaa kundi la watu wa kujitolea watakao saidiana na watumishi wa majengo ya Shekh Kuleini katika kutoa huduma mbalimbali.
- - Kuandaa kikosi cha huduma ya kwanza na uokozi pamoja na gari la wagonjwa kwa ajili ya kupambana na tatizo lolote linaloweza kutokea Allah atuepushie”.