Mawakibu za watu wa Hilla zinatoa pole kwa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Watu wa mkoa wa Hilla kutoka vitongoji tofauti wamezowea kuhuwisha msimu wa huzuni za Husseiniyya, kwa kwenda Karbala kupitia mawakibu zao za kuomboleza (Zanjiil na Matam) kumzuru bwana wa mashahidi na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), sambamba na kuomboleza kifo cha Imamu Sajjaad (a.s) kila mwaka.

Maukibu hizo huingia katika malalo mbili takatifu kwa kufuata ratiba maalum iliyo pangiwa na kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, huondoka muda huu ili wawahi kurudi katika mji wao na kujiandaa kuwahudumia mazuwaru wa Arubaini ambao hupita katika mji wa Hilla wakielekea Karbala, kuhuisha ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s).

Kutokana na watu wa Hilla kuwa na desturi ya kufanya hivyo tumeongea na kiongozi wa maukibu ya watu wa kitongoji cha Hamza mkoani Hilla bwana Thaamir Jawaad Kaadhim amesema kuwa: “Watu wa Hilla kutoka vitongoji tofauti wamezowea kuja pamoja na mawakibu za kuomboleza katika siku kama ya leo, kuomboleza kifo cha Imamu Sajjaad (a.s) na kumpa pole Imamu Swahibu Zamaan Hujjat bun Hassan (a.f) pamoja na kuomboleza kifo cha Imamu Hussein na ndugu yake mwezi wa familia Abulfadhil Abbasi (a.s)”.

Akaongeza kuwa: “Baada ya kumaliza kuomboleza hurudi haraka katika mji wa Hilla kwa ajili ya kujiandaa kuhudumia mazuwaru wa Abu Abdillahi Hussein (a.s), ambao hupitia katika mji wa Hilla wakati wa kwenda Karbala kufanya Ziara ya Arubaini, hayo ndio mazowea ya mawakibu nyingi za Hilla”.

Maukibu hizo zilianza matembezi yake katika barabara ya babu Kibla ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) hadi katika haram yake takatifu, na kumalizia matembezi yao katika malalo ya Abu Abdillahi Hussein (a.s), chini ya usimamizi wa watumishi wa kitengo cha mawakibu na vikundi vya Husseiniyya ambacho huratibu matembezi yao na kuhakikisha hayatatizi harakati za mazuwaru na hakutokei msongamano.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: