Jengo la kitivo cha udaktari katika chuo kikuu cha Alkafeel limefika hatua ya mwisho

Maoni katika picha
Shirika la Liwaau-Al-Aalamiyya chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu limefika hatua za mwisho katika ujenzi wa kitivo cha udaktari kwenye chuo kikuu cha Alkafeel, baada ya kumaliza hatua ya ujenzi wa boma la chuma na kukata vyumba.

Msimamizi mkuu wa mradi huo, Mhandisi Mustwafa Najaar amesema kuwa: “Baada ya kumaliza ujenzi wa boma la chuma na kukata vyumba kwa asilimia (%100), tulianza kufunga umeme na mifumo ya mawasiliano, kuweka mfumo wa maji taka na majisafi, mfumo wa zima moto, mfumo wa gesi na kazi zingine ambazo zimesha kamilika kwa zaidi ya asilimia (%60)”.

Akaongeza kuwa: “Shirika la Liwaau-Al-Aalamiyya ndio watekelezaji wa mradi huo”.

Tunapenda kusema kuwa chuo kikuu cha Alkafeel kwa kushirikiana na shirika la Liwaau-Al-Aalamiyya wanafanya kazi kubwa kuhakikisha wanakamilisha ujenzi huo kabla ya kuanza mwaka mpya wa masomo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: