Shehena ya vitabu mbalimbali vya turathi na utamaduni: Tawi la kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu ni alama kubwa katika maonyesho ya (Taratiilu Sajjaadiyya) ya mwaka wa saba

Maoni katika picha
Kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu kimeshiriki katika maonyesho ya (Taratiilu Sajjaadiyya) ya mwaka wa saba, kikiwa na shehena ya vitabu mbalimbali vya turathi na utamaduni.

Kiongozi wa idara ya habari na maarifa wa kitengo hicho Ustadh Ali Baasim Akabi, ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kitengo chetu kimeshiriki kikiwa na zaidi ya vitabu (200) kutoka kwenye kituo chetu na vituo vilivyo chini yetu, pamoja na machapisho ya Qur’ani tukufu kutoka kwenye Maahadi ya Qur’ani na mausua zilizo hakikiwa”.

Akaongeza kuwa: “Tumepata muitikio mkubwa kutoka kwa walimu na wanafunzi wanaojihusisha na mambo ya tafiti na historia ya umma wa kiislamu, kutokana na uzuri wa vitabu tulivyo navyo”. Tambua kuwa kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu kimesha shiriki mara nyingi kwenye maonyesho ya vitabu ya kitaifa na kimataifa, yanayo lenga kusambaza utamaduni wa kiislamu, sambamba na kumpatia msomaji vitabu anavyohitaji vya aina mbalimbali.

Kumbuka kuwa maonyesho ya (Taratiilu Sajjaadiyya) ya kimataifa awamu ya saba, yanayo simamiwa na Atabatu Husseiniyya katika eneo la katikati ya haram mbili tukufu, yaliyo funguliwa siku ya Jumatatu mwezi (25 Muharam 1442h) sawa na tarehe (14 Septemba 2020m) yataendelea kwa muda wa siku kumi, na hufanywa kila mwaka katika kumbukumbu ya kifo cha Imamu Ali bun Hussein (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: