Kuanza matembezi ya ziara ya Arubaini kutoka kusini mwa Iraq hadi Karbala

Maoni katika picha
Asubuhi ya leo mwezi (29 Muharam 1442h) sawa na tarehe (17 Septemba 2020m) yameanza matembezi ya ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s) kuelekea katika mji mtukufu wa Karbala, yameanzia katika kitongoji cha Ra-asu Bishah ni kisiwa cha Fau kisicho kaliwa na watu, kipo kusini ya mkoa wa Basra umbali wa kilometa (100) kutoka makao makuu ya mkoa, sehemu hiyo ni mpakani mwa Iraq na imefanywa na wapenzi wa Imamu Hussein (a.s) kuwa kituo cha kuanzia matembezi yao, ya kwenda kufanya ziara ya Arubaini wakitangaza kutembea (kuanzia baharini hadi mtoni) na kuifanya kuwa kauli mbiu yao.

Kikosi cha habari katika Atabatu Abbasiyya tukufu kilikuwepo eneo hilo, kama kawaida yake kinatuletea picha kuanzia mwazo kabisa wa safari hadi Karbala, kimetutumia picha kutoka katika kituo hicho ambacho kipo umbali wa kilometa (681) kutoka Karbala kwenye malalo ya Imamu Hussein (a.s), hushuhudiwa vitendo maalum vya uombolezaji sawa na tangazo la kuanza matembezi ya Arubaini, ambayo hupambwa na mambo mbalimbali yanayo ashuria uombolezaji, hushuka baharini nakutia udhu ikiwa kama ishara yakukanyaga mwisho wa ardhi ya Iraq upande wa kusini, halafu huanza safari ya kuelekea Karbala baada ya kupandishwa bendera za Husseiniyya huku wakisema kwa sauti (labbaika yaa Hussein).

Akaongeza kuwa: Kwa mwaka wa nane mfululizo linafanyika kongamano la kuanza matembezi ya Arubaini katika kitongoji cha Shaibah wilayani Fau katika mkoa wa Basra, nao ndio mji wa mwisho wa Iraq upande wa kusini, kongamano hilo huwa na kauli mbiu isemayo (kutoka baharini hadi mtoni) na hupandishwa bendera kubwa inayo ashiria kuanza kwa matembezi, na hapo watu huanza kutembea kwa miguu wakielekea Karbala kwenda kushiriki kilele cha maombolezo hayo mwezi (20) Safari, kabla ya kuanza kutembea hufanywa kongamano maalum la uzinduzi wa matembezi hayo na taasisi ya maadhimisho (Sha’aair) ambayo uko chini ya ofisi ya Marjaa Dini mkuu Sayyid Muhammad Saidi Hakim pamoja na watu wa wilaya ya Fau, maukibu za kutoa huduma hazijajitenga na eneo hilo, zinatoa huduma kwa kila mtu anaeanzia matembezi yake sehemu hiyo.

Kamera ya mpiga picha wa Alkafeel alikuwepo eneo hilo, kama kawaida yake kila mwaka hutuletea picha kuanzia mwanzo kabisa wa matembezi ya milionea.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: