Kuanza kwa kongamano la Ashura la kitamaduni awamu ya nane kwa njia ya mtandao

Maoni katika picha
Idara ya uhusiano wa vyuo na shule chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa kushirikiana na chuo kikuu cha Bagdad kupitia mradi wa kijana mzalendo wa Alkafeel, imefanya kongamano la Ashura la mwaka wa nane kwa njia ya mtandao jioni ya siku ya Ijumaa (29 Muharam 1442h) sawa na (18 Septemba 2020m), limefunguliwa kwa Quráni tukufu iliyo somwa na msomaji wa Ataba mbili takatifu Sayyid Hasanaini Halo kupitia jukwaa la (zoom), halafu ukafuata ujumbe wa kiongozi mkuu wa Kisheria Sayyid Ahmadi Swafi, ulio wasilishwa kwa niaba yake na mjumbe wa kamati kuu Dokta Abbasi Rashidi Mussawi.

Kisha ukafuata ujumbe wa mkuu wa chuo kikuu cha Bagdad Dokta Muniri Saidi, amesema kuwa: “Katika chuo cha Bagdad tunafuata misingi yote ya kitaifa, kwa ajili ya kufanikisha kila jambo zuri kwa wanafunzi wetu na taifa, mwaka huu chuo kumetengeneza toghuti ya kisasa zaidi na bado tunaendelea kutengeneza toghuti nzuri zitakazo faa vizazi vijavyo na kurahisisha ufanyaji wa tafiti za kielimu na kuitumikia jamii”.

Akaongeza kuwa: “Naishukuru Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia kiongozi wake mkuu wa kisheria Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, na ninawashukuru wasimamizi wa program hii muhimu na kubwa”.

Baada ya hapo kukawa na usomaji wa mashairi, yaliyo somwa na Dokta Ahmadi Alyawi na Saádi Shamili, kisha Muhammad Amini Tamimi akasoma tenzi.

Ikaonyeshwa filamu ya (Sayyidul-Maa), ambayo ni miongoni mwa filamu zilizo tengenezwa na Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia kituo cha Aljuud cha picha zinazo cheza kilicho chini yake.

Mwisho ikapigwa kura na kutangazwa majina ya washindi wa shindano lililoendeshwa kwa njia ya mtandao na lilikuwa sehemu ya kongamano, washindi waliopatikana ni:

Rawida Jafari Swalehe/ kutoka Maahadi ya teknik/ Karkuk.

Zahara Yahya Halul/ kitoka kitivo cha Usulu Dini.

Muhammad Abdullahi Abdulkadhim/ kutoka Chuo kikuu cha Karbala.

Saja Abduridhwa Swalehe/ kutoka Chuo kikuu cha Bagdad.

Hakimu Hamudi Salmaan/ kutoka Chuo kikuu cha Dhiqaar.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: