Vituo vya Ashura: Mwezi mosi Safar kuwasiri msafara wa mateka na vichwa katika mji wa Damaskas

Maoni katika picha
Wanahistoria wanasema kuwa mwezi mosi Safar mwaka 61 hijiriyya, msafara wa mateka na vichwa wakiwemo watoto na watu wa nyumba ya Imamu Hussein (a.s) waliwasiri Damaskas, walipo karibia kufika Ummu Kulthum alimuomba Shimri amuweke katika kundi lisilo angaliwa sana na watu, na awatoe wabebaji wa vichwa karibu yao, ili watu washughulishwe na kuangalia vichwa, walikuwa katika hali ambayo ukitaka kueleza miili inasisimka, akaamuru wawekwe katika kundi linalo angaliwa zaidi na wabeba vichwa akawaweka katikati.

Akawasimamisha mlangoni muda mrefu (masaa), watu wakatoka wanapiga dufu kwa furaha, mtu mmoja akamsogelea Sukaina akasema: nyie ni mateka wa wapi? Sukaina akasema: Sisi ni mateka wa Aali Muhammad (s.a.w.w).

Mzee mmoja akamsogelea Imamu Sajjaad (a.s) akasema: Namshukuru Mwenyezi Mungu ambae amekuangamizeni na amemuwezesha kiongozi wetu dhidi yenu, hapo Imamu akaongea kumuelelimisha yule mzee haki, hivyo ndio walivyo fanya Ahlulbait (a.s) nuru yao inaangaza na usafi wa nyoyo zao takatifu walikuwa tayali kumuongoza kila mtu. Akasema (a.s): (Ewe mzee unajua kusoma Quráni?) Akasema: ndio. Akamuuliza (a.s): (Umesoma aya isemayo (Sema: Sikuombeni malipo yeyote kwenu ila mapenzi katika kujikurubisha?) na akasoma aya isemayo (Na mpe aliye jamaa yako haki yake)? Na aya isemayo: (NA JUWENI ya kwamba ngawira mnayo ipata, basi khumsi (sehemu moja katika tano) nia ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume, na jamaa)?

Yule mzee akasema: Ndio, nimesoma aya hizo. Akasema (a.s): (Namuapa Mwenyezi Mungu sisi ndio tuliokusudiwa katika aya hizo).

Kisha Imamu akamuambia: Umesoma aya isemayo: (Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu enyi watu wa nyumba ya Mtume na kukusafisheni baarabara)? Akasema: Ndio. Akasema (a.s) (Sisi ndio watu wa nyumba ya Mtume walio takaswa na Mwenyezi Mungu). Yule mzee akasema: Unasema kweli nyie ndio watu wa nyumba ya Mtume?! Akasema (a.s): (Kwa haki ya babu yetu Mtume wa Mwenyezi Mungu sisi ndio watu wa nyumba ya Mtume, bila shaka).

Mzee akainamia miguu ya Imamu (a.s) akaanza kuibusu na huku anasema: Najitenga mbali na walio kuuweni, akaomba samahani kwa Imamu kutokana na maneno aliyokuwa amemtamkia. Taarifa hiyo ikamfikia Yazidi akaamuru mzee yule akamatwe na kuuwawa.

Yazidi alikuwa amekaa juu ya jukwaa lake, akaona mateka na vichwa vikiwa juu ya mikuki, msafara umechomeza ndio unawasiri huku kunguru wanalia, Yazidi akasoma beti zifuatazo:

Pindi zilipo chomoza zile ngamia na vikaonekana vile vichwa pembezoni mwa mji wa Jairuun.

Kunguru walilia nikasema, sema au usiseme nimelipa deni kwa Mtume.

Sahal bun Sa’adi akamsogelea Sukaina bint Hussein (a.s) akamuuliza: Unashida? Akamuambia amuamuru aliye beba kichwa aende mbali na wanawake, ili watu washughulishwe na kuangalia kichwa, Sahal akafanya hivyo.

Kabla hawajaingizwa katika kikao cha Yazidi, walifungwa kamba ambayo ilipitishwa katika shingo la Zainul-Aabidina (a.s) hadi kwa Zainabu na Ummu Kulthum na wanawake wengine wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w), kila walipo punguza mwendo katika kutembea walikuwa wanapigwa, walipelekwa hivyo hadi wakafikishwa mbele ya Yazidi, akiwa amekaa kitandani kwake, Ali bun Hussein (a.s) akasema: (Unafikiri nini atafanya Mtume wa Mwenyezi Mungu akituona tupo katika hali hii?) watu wote waliokuwepo wakalia, Yadidi akaamuru wafunguliwe.

Wakasimamishwa mbele ya mlango mkubwa sehemu ambayo husimamishwa mateka, na kichwa kitakatifu akapewa Yazidi, akawaangalia na kusema:

Tulisubiri na subira lilikuwa jambo kubwa kwetu, panga zetu zimekata watu muhimu.

Tumesambaratisha watu watukufu waliokuwa kwetu waovu na wenye dhulma.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: