Kitengo cha Dini kimemaliza ratiba ya uombolezaji ya mwezi wa Muharam katika mji wa Sanjaar na kinajiandaa na mwezi wa Safar

Maoni katika picha
Kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimetangaza kukamilika kwa ratiba ya uombolezaji, iliyo tekelezwa kwa mwaka wa nne mfululizo katika wilaya ya Sanjaar kaskazini magharibi ya mkoa wa Mosul, kupitia vituo vya maelekezo na muongozo viliyo chini ya kituo cha utamaduni, maelekezo na maendeleo.

Shekh Haidari Aaridhwi mkuu wa program hiyo, ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu mtukufu na baraka za mwenye msiba, katika kutekeleza wajibu wetu tumefuata taratibu zote za kujikinga na maambukizi, zilizo himizwa na Marjaa Dini mkuu pamoja na maagizo ya idara ya afya, ikiwa ni pamoja na kuzingatia umbali wa mtu na mtu, kuvaa barakoa, kupuliza dawa za kuuwa bakteria na mengineyo, ili kuhakikisha usalama wa afya katika mazingira haya ya janga la Korona”.

Akaongeza kuwa: “Program ilikuwa na utowaji wa mihadhara kila siku kwa nyakati tofauti, asilimia kubwa ya mihadhara imetolewa ndani ya ukumbi mkuu wa kituo na mingine imetolewa nje, na kutoa nafasi ya mihadhara maalum ya wanawake”.

Akaendelea kusema: “Mihadhara hiyo imezungumzia mambo mengi kuhusu harakati ya bwana wa mashahidi (a.s), na mafanikio yake kwa walimwengu wote, pamoja na kufasiri madhumuni yake sambamba na kuangalia mazingira yetu ya sasa, ukizingatia kuwa harakati hiyo ndio taa na shule tunayosoma kila zama na kila sehemu”.

Kumbuka kuwa kituo hakiwalengi watu fulani, bali kinawahusu wakazi wote Sunni, Shia, Turkuman, Aizidiyyina na wakurdi, kinatoa huduma mbalimbili, kama vile kutoa mihadhara, vikao vya usomaji wa Quráni, pamoja na semina za kujenga uwezo, na mambo mengine mengi kwa ajili ya manufaa ya watu wa Sanjaar, baada ya wakazi hao kupitia matatizo mengi wakati wa magaidi wa Daesh, hivi sasa tumejikita katika kujenga uwelewa wa Dini na malezi mema kwa vizazi vijavyo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: