Mgahawa wa nje wa Atabatu Abbasiyya tukufu umepandisha bendera ya kutoa huduma kwa mazuwaru wa Arubaini

Maoni katika picha
Alasiri ya leo Jumamosi (1 Safar 1442h) sawa na tarehe (19 Septemba 2020m) mwaka wa kumi na tatu mfululizo katika mgahawa wa nje ya Atabatu Abbasiyya uliopo barabara ya (Najafu – Karbala) imepandishwa bendera ya Hussein inayo ashiria kuanza rasmi kwa shughuli za kupokea mazuwaru na kuwahudumia.

Shughuli hiyo imehudhuriwa na wajumbe kadhaa wa kamati kuu ya Atabatu Abbasiyya na marais wa vitengo pamoja na kundi la viongozi wa Dini na wazee wa makabila, imefunguliwa kwa Quráni tukufu halafu ukafuata ujumbe wa Atabatu Abbasiyya tukufu ulio wasilishwa na makamo rais wa kitengo cha Dini Shekh Aadil Wakiil, ameeleza umuhimu wa kumtumikia Imamu Hussein na uwepo wa wairaq na kwamba jambo hilo ni desturi yao waliyo rithi kwa mababu zao, ukarimu walio nao kwa ajili ya Imamu Hussein (a.s) ndio alama kubwa ya utambulisho wao na hupigiwa mfano kote duniani.

Akaongeza kuwa: “Hakika Atabatu Abbasiyya tukufu imezowea kutoa huduma kwa mazuwaru wa bwana wa mashahidi na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) wakati wa ziara zao, kupitia vituo vilivyo chini yake na vilivyo kwenye barabara zinazo elekea Karbala”.

Akaongeza kuwa: “Mgahawa huu ni moja ya vituo hivyo, unatoa huduma kwa mwaka wa kumi na tatu mfululizo, tumepandisha bendera inayo ashiria ukarimu kwa mazuwaru wa Imamu Hussein (a.s) wanaotumia barabara ya (Najafu – Karbala) wanaokwenda kibla ya watu huru Imamu Abu Abdillah Hussein (a.s) kufanya ziara ya Arubaini”.

Baada ya hapo kulikuwa na utenzi uliosomwa na Shekh Aamir Khatwibu halafu ikapandishwa bendera yenye ukubwa wa mita (40) upana mita (13) na urefu mita (17) imeandikwa pande zote mbili neno lisemali: (Amani iwe juu yako ewe mbeba bendera ya Hussein).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: