Kukamilisha matengenezo ya ukuta na dari ya haram takatifu ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Kwa umaridadi mkubwa na ufundi wa kisasa na wazamani, idara ya maraya chini ya kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imemaliza kazi ya ukarabati na uwekaji wa vioo kwenye ukuta wa haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Kwa mujibu wa maelezo ya Ustadh Hassan Saidi kiongozi wa idara ya maraya, amesema kuwa: “Kazi ya kuweka vioo katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), ni miongoni mwa kazi zinazopewa kipaombele na Atabatu Abbasiyya kutokana na utukufu wa eneo hili takatifu, pia kutokana na athari ya kihandisi na kiuzuri, ukuta umewekwa vifuniko vyenye ubora mkubwa, hatua ya kwanza ilikua ni kuondoa maraya zilizo haribika na kuweka mpya za kisasa, ambazo ni nyepesi na imara zaidi, sambamba na kuzingatia muonekano wa zamani”.

Akaongeza kuwa: “Mradi huu umepitia hatua tofauti, kwanza kukarabati ukuta na paa kwa vifaa maalum, ili kuongeza uimara wake, kisha kusanifu nakshi na vioo halafu uwekaji wa vipande vya maraya, kazi hiyo ilitanguliwa na uwekaji wa nyaya za umeme, kufunga taa na kamera maalum za haram tukufu”.

Kumbuka kuwa ujenzi wote unafanywa na mafundi wa ndani ambao ni raia wa Iraq, kazi imeenda mfululizo bila kusimama na wala haikuzuwia harakati za mazuwaru, chini ya mkakati maalum wa kugawa haram sehemu tofauti.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: