Miongoni mwa maandalizi maalum ya kitengo kinacho simamia uwanja wa katikati ya haram mbili kwa ajili ya ziara ya Arubaini, ni ukarabati wa gari za kutoa huduma, kama vile gari za (usafi – maji safi – maji taka – gari za wagongwa – gari za barafu), kwa ajili ya kujiandaa kutoa huduma za uhakika wakati wa ziara.
Kwa mujibu wa maelezo ya kiongozi wa kitengo hicho bwana Haidari Yaasir Khadhwiri Hasanawi, akaongeza kusema kuwa: “Idara ya mafundi katika kitengo chetu wanafanya kazi ya kutengeneza gari hizo, pamoja na kufanya kazi hizo kila siku, kuna baadhi ya nyakati zina umuhimu zaidi, ukiwemo wakati huu ambao tunafanya matengenezo ya kila kitu, bila kusahau gari za taka ambazo zitafanya kazi ndani ya eneo lililopangwa mara tatu kwa siku, pamoja na gari za mafi safi ya kunywa (RO) na gari za barafu, ambazo hutoa huduma kwa mazuwaru na mawakibu zinazo hudumia mazuwaru, baada ya kuainisha mahitaji, tumeanza matengenezo moja kwa moja, na sasa gari zote zopo tayali kutoa huduma”.
Akasema: “Tumeandaa gari maalum za kubeba wagonjwa na kuwapeleka katika vituo vya afya vya karibu, kila gari inawahudumu wa afya pia”.
Kumbuka kuwa kitengo kinacho simamia uwanja wa katikati ya haram mbili ni sawa na vitengo vingine vya Atabatu Abbasiyya tukufu, kimejiandaa kupokea mazuwaru wa Arubaini, kimeweka mkakati maalum na kinashirikiana na kitengo cha utumishi na mitambo.