Vituo vya Ashura: Kichwa kitakatifu cha Imamu Hussein (a.s) chamkemea Yazidi kwa kusema (Laa haula walaa Quwata illaa billahi) baada ya kukichoma kwenye jicho kwa fimbo iliyokua mkononi mwake

Maoni katika picha
Wanahistoria wanasema kuwa ulipoingia msafara wa mateka wa Imamu Hussein na watu wa nyumbani kwake (a.s) katika Qasri la Yazidi –Laana iwe juu yake- lililokuwa limepambwa na kuwekwa ishara za furaha na kuandaliwa viti vya dhahabu na fedha kisha Yazidi akakaa kwenye kitanda chake, akiwa amevaa taji la duru na yaquti, huku amezungukwa na watu mia nne, wapambe wake mabalozi wake pamoja na wafalme wa kinaswara na wengineo, sambamba na mashekh wengi wa kikuraishi.

Aliagiza aletewe kichwa cha Hussein (a.s) akakiweka mbele yake katika chombo cha dhahabu, huku wanawake wakiwa wamekaa nyuma yake, Sukaina na Fatuma wakasimama wakawa wanamuangalia, Yazidi akawa anafunika macho yao, walipo kiona kichwa cha baba yao wakaanza kulia. Kisha Yazidi akaruhusu watu waingie, akachukua fimbo na akaanza kuchoma choma kichwa cha Hussein huku anasema: Leo nimelipiza siku ya Badri. Naimba na kusema Haswin bun Hamaam:

Watu wetu wamekataa kushindwa, nimeshinda sasa fimbo ipo mkononi kwangu inatoka damu.

Tumesambaratisha watu muhimu, hilo ni jambo kubwa kwetu na wao walikuwa ngome ya uovu na dhulma.

Yahya bun Hakamu bun Abi Aaswi ndugu wa Marwani alikuwa amekaa pembeni yake akasema:

Maiti zilizo lala Twafu zinaukaribu zaidi kushinda ibun Ziyadi mja muovu.

Wamekua wengi sawa na idadi ya mchanga, na Aali Mustwafa hawana ukoo.

Yazidi akampiga kifuani na akasema: Nyamaza hauna mama.

Abu Barza Aslami akasema: Hakika nilimuona Mtume anagusisha meno yake na meno ya mjukuu wake Hussein (a.s) na anasema: “Nyie ni mabwana wa vijana wa peponi, Mwenyezi Mungu amuuwe muuaji wenu, amlaani na kumuandalia moto wa Jahannam na hayo ni mafikio mabaya mno”, Yazini akakasirika akaamrisha atolewe, na akatolewa.

Mjumbe wa Qaisar akamgeukia Yazidi na akasema: Hakika sisi katika baadhi ya miji kuna unyayo wa punda wa Issa, sisi kila mwaka huenda kufanya hija kwenye nyayo hiyo na huwa tunaweka nadhiri na tunapaheshimu kama mnavyo heshimu vitabu vyenu, hakika nyie mpo kwenye batili!! Yazidi akakasirika kwa maneno hayo na akaamuru auwawe, Yule bwana akasimama na kubusu kichwa cha Imamu Hussein (a.s) na akatamka shahada mbili, wakati anauwawa watu waliokuwa wamekaa hapo wakasikia sauti kutoka kwenye kichwa kitakatifu isemayo “Laahaula walaa quwata illaa billahi” kisha walimkata kichwa wakakitenganisha na muili, halafu muili ukatundikwa kwenye Qasri kwa muda wa siku tatu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: