Maahadi ya Quráni tukufu inafanya nadwa ya Husseiniyya chini ya mwanga wa Quráni

Maoni katika picha
Maahadi ya Quráni tukufu chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu inajukumu la kufanya mambo kadhaa yenye uhusiano na kitabu cha Mwenyezi Mungu mtukufu, kwa lengo la kutambulisha madhumuni yake na kuongeza uwelewa wa kuitafakari Quráni, hivyo inaharakati mbalimbali ambozo huzifanya ili kufikia lengo hilo, ikiwa ni pamoja na kufanya nadwa za Quráni kila baada ya muda fulani.

Miongoni mwa nadwa hizo ni hii ya Husseiniyya katika mwanga wa Quráni iliyo andaliwa na tawi la Hindiyya, chini ya anuani isemayo: (Mahusiano ya islahi baina ya Quráni na Imamu Hussein (a.s)) chini ya uhadhiri wa Ustadh Abdulfataah Hasanawi katika Husseiniyya ya Abraar wilayani Hindiyya.

Ameongea kuhusu Imamu Hussein (a.s) katika mwanga wa Quráni ni Imamu wa islahi kabla ya tukio la Twafu na wakati wa tukio hilo, matunda ya harakati yake yataendelea kuonekana milele na milele.

Nadwa imehudhuriwa na wakazi wa Hindiyya pamoja na jopo la watafiti wa kisekula na baadhi ya wazee wa makabila na viongozi wa kijamii, bila kusahau wageni kutoka nje ya mji huu.

Kumbuka kuwa nadwa hii ni moja ya nadwa za Quráni zinazofanywa kila mwezi chini ya usimamizi wa Maahadi tajwa, na kila mwezi hualikwa wasomi mbalimbali wa Quráni, wa hauza na wa sekula, kwa lengo la kusambaza maarifa ya kitabu kitakatifu cha Mwenyezi Mungu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: