Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia mfululizo wa miradi ya kutoa huduma, na juhudu yake ya kusaidia sekta ya afya, hususan katika mazingira ambayo taifa linapitia kwa sasa, imetoa mtambo wa kusafisha maji (R.O station) kuipa hospitali ya watoto katika mkoa wa Karbala, ili kutatua tatizo la upungufu wa maji kwenye hospitali hiyo.
Kwa mujibu wa maelezo ya rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh, amesema: “Katika kufanyia kazi maelekezo ya Marjaa Dini mkuu, na mkakati wa Atabatu Abbasiyya wa kusaidia sekta ya afya katika mazingira ya janga la Korona, tumetengeneza kituo hiki chenye uwezo wa kusafisha (lita 1000 kwa saa), (R.O. station)”.
Akabainisha kuwa: “Mtambo wa kusafisha maji umetengenezwa kwa vifaa ghali, mtambo huo umetengenezwa Italia na vifaa vyake vimetengenezwa Marekani na vingine India, kina ubao wa kudhibiti umeme ulio tengenezwa Uswisi na vitu vingine kutoka sehemu mbalimbali, kinatenk kubwa la kuhifadhi maji linalo endana na uwezo wa uzalishaji wa kituo hicho”.
Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu inafanya miradi mbalimbali ya utoaji wa huduma, ikiwa ni pamoja na inayogusa maisha ya wananchi wa Iraq moja kwa moja, inajitahidi kutatua changamoto za wananchi kadri ya uwezo wake, miongoni mwa changamoto kubwa ambayo inapewa kipaombele ni tatizo la upungufu wa maji, jumla ya vituo vya kusafisha maji (R.O station) vilivyo jengwa na Atabatu Abbasiyya ndani na nje ya Karbala ni zaidi ya (20).