Atabatu Abbasiyya tukufu imefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu Hassan (a.s)

Maoni katika picha
Kama kawaida yake katika kuadhimisha matukio yanayo wahusu watu wa nyumba ya Mtume (a.s), Atabatu Abbasiyya tukufu imeanza uombolezaji rasmi wa mwezi wa Safar, kwa kufanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu Hassan Almujtaba (a.s), aliyekufa mwezi saba Safar, majlisi hizo zinafanywa ndani ya ukumbi wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) mkabala na mlango wa Kibla, pamoja na kufuata masharti yote yaliyo tolewa na idara ya afya na kuhimizwa na Marjaa Dini mkuu.

Majlisi hizo zitaendelea kwa muda wa siku saba, kuanzia mwanzo wa mwezi wa safar, kila siku kunamihadhara miwili, wa kwanza unatolewa saa kumi na mbili asubuhi na Sayyid Hisham Batwaat, na mhadhara wa pili unatolewa jioni na Sayyid Taisiir Mussawi, na kuhudhuriwa na watumishi wa malalo takatifu pamoja na mazuwaru, kulingana na ukubwa wa sehemu na kuzingatia ukaaji wa umbali unaotakiwa kati ya mtu na mtu.

Wazungumzaji wameeleza historia ya Imamu Hassan Almujtaba (a.s), pamoja na mambo mengi kuhusu uhai wake (a.s) na mambo aliyo ufanyia umma wa kiislamu kwa ujumla, pamoja na nafasi yake katika kuasisi harakati ya Imamu Hussein (a.s).

Sayyid Hashim Shami kiongozi wa idara ya masayyid wanaofanya kazi katika Atabatu Abbasiyya ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kila mwaka huwa tunafanya hizi majlisi za kukumbuka kifo cha Imamu Hassan Almujtaba (a.s) ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), lakini kutokana na mazingira ya mwaka huu, ya tatizo la virusi vya Korona, ambavyo tunamuomba Mwenyezi Mungu kwa Baraka za huyu tunayemkubuka atuondolee janga hili, imelazimika mwaka huu kufanya majlisi hizo kwenye eneo hili ambalo kitengo cha utumishi kimechukua jukumu la kuandaa vitu vyote vinavyo hitajika kiafya, kama vile kupuliza dawa, kuandaa barakoa na kuweka viti kwa umbali unaotakiwa”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: