Haujamzuwia umri kufanya kazi zaidi ya saa 15 mfululizo katika kuhudumia mazuwaru (angalia video).

Maoni katika picha
Mama Saad mwenye umri wa miaka themanini anasimama kuhudumia mazuwaru kwenye maukibu yake ndogo kwa muonekano kubwa kwa huduma, kuanzia saa tisa asubuhi hadi adhana ya Magharibi, akiwahudumia mazuwaru wanaokwenda Karbala kutoka mkoa wa Basra.

Mama Saad ameweka maukibu yake kaskazini ya mkoa wa Basra, anafanya kazi pamoja na watoto na wajukuu zake, amesema:

“Nilifungua maukibu hii mwaka 2003, na ilikuwa maukibu ya kwanza kutoa huduma katika njia hii, kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu na baraka za Imamu Hussein (a.s) leo hakuna sehemu ambayo ipo wazi bila kuwepo na maukibu ya kutoa huduma kwenye njia hii, jambo linalo fanywa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu hukua, ukubwa wa umri wangu haujanizuwia kufanya kazi bali kinyume chake, kumtumikia Hussein (a.s) na wafuasi wake ndio mwenendo wa Aqiilah bani Hashim (a.s), nasimama masaa kabla ya kutoka jua hadi wakati wa Magharibi, namuomba Mwenyezi Mungu anikubalie hiki kidogo”.

Sauti yake imechoka kwa kumkosa mtoto wake Shahidi, lakini haachi kuwakaribisha mazuwaru na kuwaaga kwa dua na kuwatia moyo katika safari yao, Zaidi angalia video.

Kumbuka kuwa kituo cha uzalishaji wa vipindi na matangazo mubashara Alkafeel chini ya kitengo cha habari katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimeandaa masafa ya matangazo mubashara yanayo rushwa kila siku kutokea kwenye misafara ya mazuwaru.

Ili kupata matangazo hayo katika mitandao ya habari tumia anuani zifuatazo:

Satellite: Eutelsat 7A at 7.0 East(W3A)

DOWNLINK:12680.200 H

MOD:DVBS2

QPSK

FEC:5/6

Sr :3250

HD/MPEG-4
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: