Wanafunzi wawili katika kitivo cha udaktari kwenye chuo kikuu cha Alkafeel wamepata nafasi ya kwanza na ya pili katika ngazi ya vitivo vya udaktari wa meno hapa Iraq

Maoni katika picha
Wanafunzi wawili bwana Amiir Maliki Haadi Hasuun na Ahmadi Ibrahim haatam Ibrahim wamepata nafasi ya kwanza na ya pili, katika ngazi ya wanafunzi waliohitimu udaktari wa meno hapa Iraq mwaka (2019 – 2020m) kwa kupata alama za juu kabisa kwenye mitihani yao.

Kutokana na mafanikio hayo ya kielimu tumeongea na rais wa chuo kikuu cha Alkafeel Dokta Nuris Dahaani, amesema: “Kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu na taufiq yake mwanafunzi wa kwanza kwa wanafunzi wote waliohitimu udaktari wa meno hapa Iraq ametoka katika chuo kikuu cha Alkafeel, naye ni Amiir Maliki Haadi Hasuun, na rafiki yake Ahmadi Haatam Ibrahim akawa mshindi wa pili, baada ya kupata alama za juu kabisa katika mitihani ya kuhitimu masomo, inayo fanywa na vyuo vyote binafsi vya udaktari wa meno hapa Iraq”.

Akaomngeza kuwa: “Tunawapongeza wao na wahitimu wote wa udaktari wa meno katika chuo kikuu cha Alkafeel, jambo hili linaonyesha ufundishaji mzuri wa chuo cha Alkafeel, unaotokana na umahiri na uwezo mkubwa walionao walimu wetu, pamoja na juhudi za wanafunzi wetu”.

Kumbuka kuwa chuo cha Alkafeel kinafanya kila kiwezalo kuhakikisha kinatoa huduma bora za elimu, utamaduni, malezi na tafiti za kielimu hapa Iraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: