Yeyote katika sisi atakufa kwa sumu au kwa kuuwawa: mwezi saba Safar ni kumbukumbu ya kifo cha Imamu Hassan (a.s)

Maoni katika picha
Wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s) katika siku kama ya leo mwezi saba Safar wanaomboleza msiba mkubwa ulioikumba nyumba ya Utume na wahyi, ambao ni kifo cha Imamu Hassan Almujtaba (a.s) mjukuu wa Mtume (s.a.w.w) na bwana wa vijana wa peponi, aliye lelewa katika mazingira ya kushushwa wahyi na akanyonya maziwa matakatifu ya mbora wa wanawake wa peponi (a.s).

Shekh Mufiid (r.a) anasema: walipo fanya sulhu baina ya Hassan (a.s) na Muawiya, Imamu Hassan (a.s) alikaa Madina akisubiri amri ya Mola wake mtukufu, hadi Muawiya akafikisha miaka kumi ya utawala wake na kampa baiyya (ahadi ya uongozi) mtoto wake Yazidi, jambo hilo lilikua kinyume na makubaliano ya sulhu baina yao, akawa anaogopa majibu ya Imamu kwa kitendo cha yeye kuvunja makubaliano ya sulhu ndio akaamua kumuua.

Akampa sumu kupitia Juúdah binti Asháth bun Qais mke wa Imamu Hassan (a.s), --sumu hiyo aliitoa kwa mfalme wa Rum-, akamuahidi kuwa atamuozesha mwanae Yazidi na akampa dirham elfu moja. Juúdah akampa sumu mumewe, akaugua kwa muda wa siku arubaini na akafa ndani ya mwezi wa Safar mwaka wa hamsini hijiriyya akiwa na miaka arubaini na nane.

Ndugu yake Hussein (a.s) akashughulikia maziko yake, akamuosha na kumsha sanda kisha akaenda kumzika karibu na bibi yake Fatuma bint Asadi bun Hashim bun Abdulmanafi (r.a) katika makaburi ya Baqii.

Kuna riwaya inasema kuwa: Muili wa Imamu (a.s) ulishambuliwa mishale hadi ikafika sabini, banu Hashim wakataka kujibu, Imamu Hussein (a.s) akawaambia: Allah.. Allah.. msivunje usia wa ndugu yangu, hakika alisisitiza kuwa kama nikizuiliwa kumzika karibu na babu yake (s.a.w.w) nisibishane na yeyote. Kama sio usia wake mngeona namna gani namzika pembeni ya Mtume (s.a.w.w), ndio wakaenda kumzika Baqii pembeni ya kaburi la bibi yake Fatuma bint Asadi (a.s).

Abu Faraji anasema: Alipokufa Hassan bun Ali (a.s) na kutolewa jeneza lake Marwani alilibeba, Hussein (a.s) akamuambia: unabeba jeneza lake? Wewe si ulikua unamchukia. Maruwani akasema: Nilikua namchukia mtu ambae uzito wake sawa na jabali.

Ibun Shahri Aashubu amepokea kuwa: Hussein (a.s) alipo muweka ndugu yake Hassan (a.s) kaburini alisema:

Nipake mafuta kichwa change au nijipendezeshe wakati kichwa chako kipo kwenye vumbi.

Nitalia sana machozi mengi yatatoka na wewe uko mbali na mazaru ipo karibu.

Ibun Abbasi amepokea hadithi kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kuhusu utukufu wa kumlilia na kumzuru, anasema: “… Mambo yataendelea hadi atakapo uwawa kwa sumu akiwa mwenye kudhulumiwa na kufanyiwa uadui, hapo ataliliwa na malaika pamoja na mbingu saba kwa kifo chake, ataliliwa na kila kitu hadi ndege wanaoruka angani na samaki ndani ya maji, atakae mlilia macho yake hayatapofuka siku ambayo macho yatapofuka, na atakae mhuzunikia hatahuzunika siku ambayo nyoyo zitahuzunika, atakaemtembelea Baqii miguu yake haitatereza kwenye Swiraat siku ambayo miguu itatereza”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: