Mawakibu za kuomboleza za Karbala zinampa pole Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa kifo cha ndugu yake Imamu Hassan (a.s)

Maoni katika picha
Tangu asubuhi mawakibu za watu wa Karbala zimeanza kumiminika kuja kumpa pole Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa msiba mkubwa uliopata nyumba ya Mtume katika siku kama ya leo mwezi saba Safar mwaka wa Hamsini Hijiriyya, kwa kuuwawa mjukuu na kipenzi wa Mtume Imamu Hassan (a.s), kumbukumbu ya kifo chake imesadifu siku ya Ijumaa mwezi (7 Safar 1442h), kama kawaida ya maukibu hizo katika kuhuisha kumbukumbu za tarehe za vifo vya maimamu watakasifu (a.s), utamaduni ambao wamerithi kizazi baada ya kizazi, lakini mwaka huu umekua tofauti na miaka mingine kutokana na kuwepo kwa janga la virusi vya Korona.

Makamo rais wa kitengo cha mawakibu na vikundi vya Husseiniyya katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya Sayyid Hashim Mussawi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Hakika kuomboleza kifo cha Imamu Hassan Almujtaba (a.s) ni miongoni mwa utamaduni wa mawakibu na vikundi vya Husseiniyya katika mkoa wa Karbala, mawakibu za waombolezaji zimeanza matembezi tangu asubuhi, zikielekea kwenye malalo ya bwana wa mashahidi na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), kuwapa pole kwa msiba huu mkubwa ulioikumba nyumba ya Ahlulbait (a.s) na wapenzi wao katika siku kama ya leo”.

Akaongeza kusema: “Kitengo chetu kimeandaa mkakati wa kupokea mawakibu zitakazo kuja kuomboleza msiba huu, tumeainisha njia zake na sehemu matembezi yatakapo anzia na kuishia, na kutekeleza masharti yote yaliyotolewa na idara ya afya, sambamba na kuhakikisha hakuna msongamano katika matembezi, tumeweka watumishi wanaosaidia kuongoza matembezi njia nzima, kuanzia mwanzo hadi mwisho”.

Kumbuka kuwa matembezi ya mawakibu hizi yanaanzia kwenye barabara inayo elekea kwenye haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), hadi kwenye haram hiyo, wakiwa wamesimama kwa mistari na kuimba kaswida za huzuni, baada ya kuingia kwenye malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) wanaelekea kwenye malalo ya bwana wa mashahidi (a.s) wakipitia katika uwanja wa katikati ya haram mbili takatifu, wakiwa wanaimba na kupiga matam.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: