Vituo vya Ashura: Kichwa kitakatifu cha Imamu Hussein (a.s) kiliwekwa sehemu tatu katika mji wa Damaskas

Maoni katika picha
Riwaya zinasema kuwa Yazidi –laana iwe juu yake- baada ya kumaliza kuangalia kichwa cha Hussein (a.s) na vichwa vingine vya watu wa nyumba ya Mtume (a.s), aliamuru vipelekwe sehemu tatu kwa mpangilio ufuatao:

  • - Kwenye mlango wa Qarsi yake.
  • - Kisha kwenye mlango wa Damaskas.
  • - Kisha kwenye mlango wa msikiti mkuu (Masjid Jaamiá).

Kichwa cha Hussein (a.s) alikiweka kwenye mlango wa Qasri yake kwa muda wa siku tatu, mke wake akachukizwa na kitendo hicho, akakitoa na kukipeleka kwenye mlango wa Damaskas, halafu akakitoa na kukiweka kwenye chumba chake cha kulala kwa usiku mmoja, Hindu –mke wa Yazidi- akaamka usiku na kuona nuru kuanzia chumbani kwao hadi mbinguni, akamuambia mumewe kua anaongoka, ndio Yazidi akatoa kichwa hicho na kukiweka kwenye mlango wa msikiti, au juu ya mnara wa msikiti mkuu wa Damaskas.

Vichwa vingine viliwekwa kwenye mlango wa Qasri, na vikakaa siku kadhaa kwenye mlano wa mji –Damaskas- kisha vikawekwa kwenye mlango wa masjid Jaamiá.

Muqarramu anasema kuwa, baada ya kutoa kichwa kwenye kikao (majlisi), kiliwekwa juu ya mlango wa Qasri kwa muda wa siku tatu, Yazidi akaamuru vichwa vingine viwekwe kwenye mlango wa Damaskas na kwenye jengo la Umawiyya, wakafanya hivyo.

Bibi Hindu binti Amru bun Suhaili mke wa Yazidi, alipo ona kichwa kikiwa kwenye mlango wa nyumba yake na nuru ya Mwenyezi Mungu inaangaza, huku kikiwa kinavuja damu mbichi, bado haijakauka, na kinatoa harufu nzuri, aliingia kwenye kikao akiwa amevaa hijabu, akamvamia Yazidi na kumuambia: Kichwa cha mtoto wa binti wa Mtume wa Mwenyezi Mungu kinasulubiwa katika nyumba yetu?!. Yazidi akasimama na kukifunika, akasema: Nisamehe ewe Hindu, hakika zilikua fujo za bani Hashim, Ibun Ziyadi akafanya haraka akamuuwa, Mungu atamlaani.

Kichwa cha Imamu Hussein (a.s) kilisulubiwa sehemu kilipo sulubiwa kichwa cha Yahya (a.s).

Katika kitabu cha (maisha ya Imamu Hussein) kilicho andikwa na Shekh Baaqir Sharifu Quraishi (r.a) imendikwa kuwa: Baada ya Yazidi kuchezea kichwa cha bwana wa vijana wa peponi, alikitundika katika Jaamiá Damaskas, sehemu kilipo tundikwa kichwa cha Nabii Yahya mtoto wa Zakariya (a.s), kwa muda wa siku tatu.

Katika kibatu cha (Taqwimu Buldani) cha Abu Fidaau kimeandika kuwa, alipo uwawa Yahya bun Zakariya (a.s), kichwa chake kilitungikwa kwenye mlango wa msikiti unao itwa Baabu Jairuun, na kwenye mlango huo huo kikatungikwa kichwa cha Hussein (a.s) pale pale kilipo tungikwa kichwa cha Yahya bun Zakariya (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: