Maukibu Ummul-Banina (a.s) imetangaza kukamilisha maandalizi ya kupokea mazuwaru wa Arubaini

Maoni katika picha
Maukibu Ummul-Banina (a.s) iliyopo katika barabara ya (Najafu / Karbala) kituo cha –Chuo kikuu cha Al-Ameed- chini ya usimamizi wa chuo hicho, imetangaza kuwa imekamilisha maandalizi yote ya kupokea mazuwaru wa Arubaini katika sekta zote na maeneo yote yaliyo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu.

Makamo rais wa chuo Dokta Alaa Mussawi amesema kuwa: “Kufuatia maelekezo ya Atabatu Abbasiyya tukufu na uongozi wa chuo na mkakati wa kupokea mazuwaru wa Arubaini, maukibu ya Ummul-Banina (a.s) chini ya chuo kikuu cha Al-Ameed ilianza maandalizi mapema, imeweka mapambo yanayo ashiria huzuni sehemu zote, na imejenga hema za kutolea huduma upande wa wanaume na wanawake, hali kadhalika imeandaa kumbi za chuo na kuweka mahitaji yote muhimu kwa ajili ya kulala mazuwaru”.

Akaongeza kuwa: “Maukibu imetenga sehemu kwa ajili ya kuelekeza mazuwaru na kusaidia waliopotelewa pamoja na sehemu ya kutolea huduma za afya, aidha kuna ukumbi maalum kwa ajili ya tablighi na maelekezo ya kidini, pia kuna sehemu ya vyoo na ukumbi wa chakula, pamoja na kufunga mitambo ya kupuliza dawa mazuwaru kwa ajili ya kuwakinga na maambukizi ya virusi vya Korona”.

Akasisitiza kuwa: “Tumechukua tahadhari zote za kiafya kwa ajili ya usalama wa watumishi wa mazuwaru watukufu”.

Kumbuka kuwa maukibu hii ni sehemu ya vikundi vya Husseiniyya vilivyo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, ambayo imekua ikihudumia mazuwaru kwa miaka mingi na bado inaendelea kutoa huduma, pamoja na kuwa ipo ndani ya chuo kikuu cha Al-Ameed ambacho kipo chini ya Atabatu tukufu, jambo hili halijazuwia utoaji wa huduma, bali ndio imeongeza uwezo wa kutoa huduma kutokana na kuwezeshwa na chuo upande wa vitendea kazi vya kuhudumia mazuwaru.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: