Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya inaomboleza kifo cha bibi Ruqayyah (a.s)

Maoni katika picha
Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya tawi la wanawake, chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, inaomboleza kifo cha bibi Ruqayyah (a.s) kwa mwaka wa kumi mfululizo, chini ya ratiba maalum ya uombolezaji ndani ya ukumbi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) na kuhudhuriwa na kundi kubwa la mazuwaru.

Majlisi hiyo imefunguliwa kwa Quráni tukufu, ukafuata muhadhara kuhusu bibi Ruqayyah (a.s) na shida alizo pitia katika msafara wa mateka, wakahitimisha kwa utenzi ulioeleza kisa cha kifo chake (a.s), baada ya hapo likafuata igizo, halafu ikaibwa kaswida na kundi la watoto waliofanya igizo.

Kwa mujibu wa maelezo ya makamo kiongozi wa idara hiyo bibi Taghridi Tamimi kwa mtandao wa Alkafeel, amesema: “Hakika idara ya wahadhiri inaendelea na majlisi za Husseiniyya tangu siku ya kwanza ya mwezi wa Muharam hadi leo, ikiwa ni pamoja na program ya kuomboleza msiba huu”.

Akasema kuwa: “Program zote zinafanywa kwa kuzingatia masharti ya afya na mada zote zinalenga kueneza utamaduni wa Husseiniyya katika jamii, kwa namna inayo endana na umuhimu wa tablighi sambamba na kuomboleza kifo cha kipenzi wa Imamu Hussein (a.s)”.

Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu inafanya juhudi za kuhakikisha msimu wa Ashura ya Imamu Hussein (a.s) kuwa msimu wa mafundisho mema ya kiislamu kwa wanawake kupitia majukwaa yao rasmi, idara ya wahadhiri wa Husseiniyya ni moja ya majukwaa hayo, imeendelea kutekeleza majukumu yake pamoja na kufanyia kazi maelekezo ya idara ya afya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: