Vituo vya Ashura: Bibi Zainabu (a.s) ashuku uislamu wa Yazidi naye mal-uuni akasirika

Maoni katika picha
Bibi Zainabu anamisimamo mingi isiyo isha, kabla ya tukio la Twafu au baada yake, katika msafara wa mateka ambao yeye alikua sawa na mshika bendera na mlinzi wa familia ya kaka yake na watu wa nyumbani kwake kutokana na hatari yeyote ambayo wangeipata, yeye alikua ngome imara pamoja na mitihani yote aliyopata na aliyo shuhudia, ikiwa ni pamoja na msimamo alio onyesha katika kikao cha Yazidi (laana iwe juu yake) huko Sham.

Sayyid Amiin katika kitabu cha (Lawaaij Ashjaan) ameandika kuwa, walipo ingia wanawake (mateka kutoka msafara wa Imamu Hussein –a.s- na watu wa nyumbani kwake) kwa Yazidi, mtu mmoja wa Sham alimuangalia Fatuma bint Hussein (a.s), kisha akamuambia Yazidi: Ewe kiongozi wa waumini, nipe huyu mateka, hakika wao kwetu ni halali.

Fatuma akasema: Nikaogopa na nikadhani hilo linafaa kwao, nikajificha kwenye nguo ya shangazi yangu Zainabu, na nikasema: ewe shangazi yangu, nimefanywa yatima na sasa nimekua mtumwa?!. Shangazi alikua anajua kua hilo haliwezi kutokea, shangazi akasema: hakuna mapenzi wala utukufu kwa huyu muovu. Kisha akamuambia yule mtu: umesema uongo na umekosea, wallahi hilo haliwezekani kwako wala kwake.

Yazidi akachukia na akasema: Hilo lipo ndani ya uwezo wangu, nikitaka naweza kufanya.

Zainabu (a.s) akasema: Hapana.. hauwezi kufanya hivyo ispokua ukitoka katika mila yetu na uingie dini nyingine. Katika kitabu cha (Tadhkirah Khawaaswi) cha ibun Jauzi… alisema: Swali kwa kuelekea kibla nyingine, na uingie dini nyingine, na ufanye utakavyo.

Yazidi akachukia, na akasema: Unanikabili kwa maneno kiasi hicho?. Hakika baba yako na kaka yako walitoka katika dini.

Bibi Zainabu (a.s) akasema: Nimeongoka kwa dini ya Allah na dini ya baba yangu na babu yangu, labda wewe na baba yako na babu yako kama kweli ni uislamu.

Akasema (Yazidi): Umedanganya ewe adui wa Mwenyezi Mungu. Akasema (Zainabu –a.s-): Wewe ni kiongozi anatukana aliye dhulumiwa, na unatumia ufalme wako!.

Ibun Jauzi anasema: Namuapa Mwenyezi Mungu aliona aibu akanyamaza.

Kisha yule mtu akarudia kusema, ewe kiongozi nipe huyu mateka. Yazidi akamuambia: Acha, Mwenyezi Mungu ameshakupa mke.

Katika riwaya ya ibun Twausi, mtu huyo alisema: Huyu mateka ni nani?

Yazidi akasema: Huyu ni Fatuma mtoto wa Hussein, na yule ni Zainabu mtoto wa Ali bun Abu Twalib. Yule mtu akasema: Hussein mtoto wa Fatuma na Ali mtoto wa Abu Twalib? Akasema: ndio, yule mtu akasema: Mwenyezi Mungu akulaani ewe Yazidi, unauwa kizazi cha mtume wako na unateka familia yake!. Wallahi nilidhani ni mateka kutoka Ruum.

Yazidi akasema: Wallahi nitakuunganisha nao, akatoa amri akatwe shingo lake (akauwawa).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: