Kuanza kwa shindano la (Mtunzi mdogo) la kuandika visa vya tukio la Twafu la Husseini

Maoni katika picha
Kituo cha utamaduni wa familia katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimeanza shindano la (Mtunzi mdogo) la kuandika visa kuhusu tukio la Twafu, washiriki ni watoto wenye umri wa miaka (8 / 12) wa jinsia zote mbili, kufuatia kumbukumbu ya tukio la Twafu na matembezi ya Arubaini, ili kukuza vipaji vya kundi hilo muhimu, sambamba na kubaini vipaji vyao na kuangalia njia sahihi za kuviendeleza.

Kiongozi wa idara hiyo Ustadhat Asmahani Ibrahim amesema kuwa: “Hili ni moja ya mashindano ya kitamaduni yanayo simamiwa na kituo katika kipindi hiki, tunatumia nafasi waliyo nayo watoto kufanya mambo yenye faida kwao, na kuongeza mafungamano kati yao na tukio la Imamu Hussein (a.s), pamoja na kuonyesha kuathirika kwao kuhusu tukio hilo na kulielezea kupitia visa kwa njia inayo endana na umri wao, ikiwa pia ni sehemu ya kuwashajihisha waipende lugha ya kiarabu na utamaduni wake kupitia mwenendo madhubuti wa Husseiniyya”.

Akaongeza kuwa: “Shindano litadumu kwa muda wa siku kumi, tutatoa zawadi kwa washindi watatu wa mwanzo, baada ya kuchuja kazi zao na kuzisaili chini ya kamati ya majaji walio bobea”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: