Zaidi ya watu laki mbili wamefanyiwa ziara kwa niaba ndani ya mwezi wa Muharam na maandalizi ya ziara ya Arubaini bado yanaendelea

Maoni katika picha
Idara ya taaluma chini ya kitengo cha Atabatu Abbasiyya tukufu, imesema kuwa dirisha la ziara kwa niaba kwenye mtandao wa kimataifa Alkafeel, imepokea na kufanya ziara kwa niaba za watu zaidi ya laki mbili kutoka nchi tofauti duniani, kupitia mitandao yake ya (kiarabu – kiingereza – kifarsi – kituruki – ki-urdu- kifaransa – Kiswahili na kijerumani) ndani ya mwezi wa Muharam, maandalizi ya kuanza ziara ya Arubaini yanaendelea.

Hayo yamesemwa na Ustadh Haidari Twalibu Abdul-Amiir kiongozi wa idara tajwa, akaongeza kuwa: “Kutokana na mazingira ya sasa ambayo dunia inapitia kwa ujumla pamoja na Iraq, ya tatizo la virusi vya Korona linalo sababisha idadi kubwa ya watu kushindwa kuja kufanya ziara kwenye malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), dirisha hili limepokea maombi mengi kutoka kila sehemu ya dunia, hivyo tumeweka mkakati maalum wa kuwafanyia ziara katika mwezi wa Muharam na Safar”.

Akaongeza kuwa: “Mwezi wa Muharam ulikua na ziara nyingi, siku kumi za kwanza tulizitenga kwa ajili ya ziara ya Imamu Hussein -a.s- (ziara ya Ashura) na ziara ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na tukamalizia kwa ziara maalum ya mwezi kumi Muharam, kisha zikaendelea ziara za masiku ya Ijumaa, ndugu zetu masayyid wanaofanya kazi katika Atabatu Abbasiyya ndio waliofanya ziara hizo”.

Akasema: “Kulikua na ziara ya Imamu Zainul-Aabidina (a.s) katika kumbukumbu ya kifo chake mwezi ishirini na tano Muharam, iliyo fanywa katika mji wa Madina na ndugu zetu waliojitolea katika mji huo”.

Akaendelea kusema: “Kulikua na muda mrefu wa kutangaza ziara hizi, ili kutoa nafasi ya kupokea maombi mengi zaidi, asilimia kubwa ya watu walio fanyiwa ziara wametoka katika nchi zifuatazo: (Iraq, Iran, Lebanon, Bakistani, Urusi, Marekani, Uingereza, India, Saudia, Swiden, Kanada, Kuwait, Malezia, Australia, Aljeria, Baharain, Misri, Ujerumani, Oman, Ekwado, Brazili, Ajentina, Uswisi, Naijeria, Gana, Yemen, Indonesia, Italia, Hispania, Ufaransa, Uturuki, Adharbaijan, Qabrus, Finland, China, Ealend, Honkon, Japani, Falme za kiarabu, Sudani)”.

Akamaliza kwa kusema: “Tunaendelea kujiandaa kwa ajili ya kufanya ziara kwa niaba kupitia dirisha letu, na tunatarajia kufanya kwa namna bora zaidi kushinda mara ya kwanza, kutokana na mazingira ya sasa ambayo idadi kubwa ya watu wameshindwa kuja kufanya ziara”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: