Kamanda wa polisi wa mkoa wa Karbala ametembelea kitengo cha mawakibu na vikundi vya Husseiniyya na amepongeza ushirikiano wao na vyombo vya ulinzi na usalama

Maoni katika picha
Kamanda wa poli wa Karbala Ahmadi Zawini amesifu ushirikiano unao onyeshwa na kitengo cha mawakibu na vikundi vya Husseiniyya chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama kupitia kikosi cha ulinzi wa haram mbili tukufu, kwa namna ambayo wamepangilia matembezi na uingiaji wa mawakibu za kuomboleza pamoja na za kutoa huduma, zinazo shiriki kwenye ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s).

Aliyasema hayo alipo tembelea ofisi za kikosi cha ulinzi wa haram mbili ambayo ipo chini ya polisi wa Karbala, kinacho husika na kupangilia na kusimamia matembezi ya mawakibu za waombolezaji na za kutoa huduma zinazo shiriki kwenye ziara ya Arubaini mwaka huu, na kuwapa vitambulisho maalum.

Makamo rais wa kitengo Sayyid Hashim Mussawi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Amefanya ziara hii kukagua maandalizi ya kupokea mawakibu zitakazo miminika katika mji wa Karbala ndani ya siku hizi, pamoja na kuangalia utekelezaji wa kanuni maalum za mawakibu, na amehimiza umuhimu wa kuendelea kuwa na mawasiliano ya karibu na kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya ili kuhakikisha zowezi hili linafanyika vizuri”.

Akafafanua kuwa: “Miongoni mwa maandalizi maalum ni kugawa vitambulisho kwa viongozi wa mawakibu, jambo hilo ni muhimu zaidi kisheria na kimpangilio, ili kuzitambua mawakibu zinazo shiriki kwenye ziara ya Arubaini na kudhibiti utendaji wake na harakati zake kwa kushirikiana na mamlaka husika pamoja na polisi wa Karbala”.

Kumbuka kuwa kitengo cha maadhimisho kinajukumu la kupangilia shughuli za mawakibu na vikundi vya Husseiniyya kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama, taasisi za kijamii na kiraia ambazo husaidia mawakibu na vikundi vya Husseiniyya kutoa huduma wao ni wahisani tu, haziwajibiki kisheria kupangilia utendaji wa maukibu hizo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: