Kitengo cha utumishi kimeanza kutekeleza mkakati maalum wa ziara ya Arubaini

Maoni katika picha
Kitengo cha utumishi chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu kimeanza kutekeleza mkakati maalum wa kuhudumia mazuwaru wa Abu Abdillahi Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) katika ziara ya Arubaini, kupitia idara zote za kitengo hicho, zinazo lenga kutoa huduma bora kabisa kwa mazuwaru na kuhakikisha wanafanya ziara katika mazingira bora na kwa urahisi.

Makamo rais wa kitengo cha utumishi Mhandisi Abbasi Ali ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Tumeanza kutekeleza mkakati wetu maalum wa ziara ya Arubaini, tunahuduma nyingi na za aina mbalimbali tunazotoa kwa mazuwaru wa bwana wa mashahidi na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s)”.

Akaongeza: “Tutaongeza tenki na maji ya kunywa sambamba na kuendelea na kazi ya kusafisha maeneo yanayo zunguka Atabatu Abbasiyya tukufu, na kuandaa vivuri sehemu za kutunzia viatu na vitu pamoja na sehemu maalum za kulala wahudumu wanaojitolea, sambamba na kuweka vyoo vya dharura katika barabara zote zinazo ingia hapa mkoani na ndani ya mji mtukufu wa Karbala, bila kusahau utekelezaji wa kanuni za afya kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya magonjwa”.

Akaendelea kusema: “Majengo yote ya vyoo yaliyo chini ya kitengo chetu yapo tayali kutoa huduma, hali kadhalika magari na vifaa vyote vipo tayali kwa ajili ya kufanya kazi mbalimbali”.

Akasema: “Itaongezeka kati ya kupuliza dawa za kujikinga na maambukizi wakati wa ziara sambamba na kuhakikisha tahadhari zote za kujikinga na maambukizi zinafatwa”.

Kumbuka kuwa kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya tukufu ni miongoni mwa vitengo ambavyo hutoa huduma za moja kwa moja kwa mazuwaru, na hufanya kila kiwezalo katika kuhakikisha kinatoa huduma bora zaidi kwa zaairu, sawa iwe ndani ya Ataba au nje, kitengo kina watu wengi wanaofanya kazi kwa kujitolea, utawakuta wanafanya kazi bega kwa bega na watumishi wa kitengo hicho katika kuwahudumia mazuwaru.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: