Kazi ya kuweka zaidi ya vituo 45 vya kuongoza waliopotea na kupotelewa imekamilika

Maoni katika picha
Idara ya mawasiliano na teknolojia chini ya kitengo cha miradi katika Atabatu Abbasiyya tukufu imekamilisha kazi ya kuweka Zaidi ya vituo (45) vya kuongoza waliopotea na kupotelewa katika ziara ya Arubaini, vituo hivyo vimewekwa kwenye barabara kuu zinazo elekea Karbala, upande wa mkoa wa Baabil, Najafu na Bagdad.

Kwa mujibu wa maelezo ya kiongozi wa idara hiyo Mhandisi Farasi Hamza, amesema: “Vituo hivyo vinajukumu la kuelekeza mazuwaru waliopotea na kusaidia walio potelewa, hususan watoto na wazee na kuhakikisha wanakutana na jamaa zao, wanatumia njia za kisasa zitakazo rahisisha watumishi wa vituo hivyo kutekeleza jukumu lao, kazi hiyo itafanywa na watu wanao jitolea kutoka katika mradi wa kijana mzalendo wa Alkafeel chini ya idara ya mahusiano ya vyuo na shule katika Atabatu Abbasiyya tukufu, amesema kuwa kila kituo kina vitu vifuatavyo:

  • - Simu na intanet kwa ajili ya kuwasiliana na vituo vingine kwa urahisi.
  • - Kompyuta yenye program maalum inayo onganisha vituo vyote kwa njia ya mtandoa kiasi unapo andika taarifa ya mtu aliyepotea inaonekana kwenye vituo vyote, pia kompyuta hiyo imeonganishwa na chumba kikuu cha ukaguzi.
  • - Imewekwa Screen kubwa juu ya mlango wa kila kituo inayo onyesha, jina, umri na anuani ya mtu aliyepotea.
  • - Kipaza sauti kwa ajili ya kutangaza waliopotezana.
  • - Gari maalum itakayo kuwa inazunguka kwenye vituo hivyo kwa ajili ya kuchukua waliopotea na kuwapeleka kwa jamaa zao au kwenye kituo kikuu cha kuhifadhi walio potea.
  • - Ukurasa wa utambulisho utakao andikwa taarifa za mtoto au mzee (mtu) aliyepotea pamoja na anuani yake na namba ya simu, ili kila kituo kiweze kumfahamu kwa wepesi na kuweka taarifa zake kwenye vituo vyote.

Akafafanua: “Vituo vyote vimeunganishwa na mtandao maalum wa simu, na mawasiliano yote yameunganishwa na chumba kikuu cha ukaguzi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, ambacho kinatunza taarifa zote za watu waliopotea, wataalamu wa kitengo hicho wametengeneza hifadhio (seva) maalum kwa ajili ya kuhifadhi taarifa zitakazo toka kwenye vituo hivyo tu”.

Kumbuka kuwa vitengo vyote vya Atabatu Abbasiyya na idara zake, zimefanya maandalizi makubwa kwa ajili ya kupokea watu wanaokuja kufanya ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), na idara ya mawasiliano ni moja ya idara ambazo zimejiandaa vizuri, na miongoni mwa maandalizi yake ni utengenezaji wa vituo hivi vya kusaidia waliopotea au kupotelewa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: