Waasit imeitikia wito wa Arubaini na inaelekea kibla ya wapenzi

Maoni katika picha
Mkoa wa Waasit ni sawa na mikoa mingine ya kusini, wapenzi na wafuasi wa Imamu Hussein (a.s) wameanza kutembea kuelekea Karbala kuhuisha ahadi yao kwa Abu Abdillahi Hussein (a.s).

Kwa mujibu wa maelezo ya mgeni wa mtandao wa Alkafeel katika mkoa huo, amesema kuwa mwaka huu matembezi yameanza mapema, kwani mkoa huo ni makutano kuu ya watu wanaotoka mkoa wa Misaan, kisha hugawanyika katika barabara mbili kuu, ya kwanza inapita kwenye mkoa wa Qadisiyya (Diwaniyya), na kupita kwenye mikoa mingine ya kusini, matembezi yao katika mikoa hiyo hupita pembezoni ya mto wa Dujla, kundi la pili hupita barabara nyingine hadi mkoa wa Baabil kisha huelekea Karbala.

Akabainisha kuwa wakazi wa mkoa huu pamoja na mawakibu Husseiniyya wamesha anza kutoa huduma kwa mazuwaru kama kawaida yao kila mwaka, wanagawa chakula, vinywaji na kuandaa sehemu za kupumzika mazuwaru, wanagawa vyakula vya aina tofauti katika milo yote mitatu, huduma hizo zinaenda sambamba na uimarishaji wa ulinzi na usalama pamoja na utoaji wa huduma za afya chini ya idara ya mkoa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: