Mpangokazi wa kituo cha faharasi na kupangilia taaluma umeingizwa katika mpango wa umoja wa mataifa wa maendeleo endelevu kama mpango kazi bora wa Iraq

Maoni katika picha
Kituo cha faharasi na kupangilia taaluma chini ya maktaba na daru makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu kitengo cha habari na utamaduni, kimesema kuwa umoja wa mataifa umeingiza mpango kazi waliotumia wakati wa janga la Korona, katika mipango yake maalum ya maendeleo endelevu 2030 kama mpango bora wa Iraq kwa miaka miwili mfululizo.

Yamesemwa na mkuu wa kituo Ustadh Hasanaini Mussawi, akaongeza kuwa: “Katika kipindi kilicho pita tumeratibu mipangokazi (17) tofauti, ya kitaifa kikanda na kimataifa, lakini mpango kazi wetu haukusimama katika kipiti ambacho mipangokazi mingine ilisimama kutokana na janga la maambukizi ya virusi vya Korona, uliendelea kama kawaida kwa kutumia njia za kielektronik, tulikuwa wa kwanza kunufaika na muda na kupata mafanikio mazuri”.

Akaongeza kuwa: “Umoja wa muungano wa jumuiya za maktaba na vituo vya elimu (IFLA) umechukulia kuwa mpangokazi bora wa Iraq chini ya vigezo maalum wanavyo tumia, baada ya kuukagua na kuangalia faida zake, kisha wakauingiza katika mpango kazi maalum wa umoja wa mataifa chini ya malengo endelezu ya 2030, sasa utaangaliwa pamoja na mipango mingine kila mwaka”.

Akamaliza kwa kusema: “Hakika mafanikio yaliyopatikana yanatokana na juhudi za watumishi wa kituo pamoja na ufanisi wao katika kazi, baada ya kuandaliwa mazingira mazuri na Atabatu Abbasiyya, tunaendelea kutekeleza mradi huu chini ya mpangokazi uliowekwa”.

Kumbuka kuwa kituo cha faharasi na kupangilia taaluma kinaendelea kufanya kazi zake kwa njia ya mtandao, na kimetengeneza program yake maalum yenye mambo yote muhimu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: