Chuo kikuu cha Alkafeel kupitia rais wake Dokta Nuris Dahani na chuo kikuu cha Al-Ameed kupitia rais wake Dokta Muayyad Ghazali, chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, wamehudhuria mkutano wa vyuo vikuu binafsi vya Iraq, ulioandaliwa na kamati ya kusimamia ubora wa elimu kutoka wizara ya elimu na utafiti, ikiwa ni katika maandalizi ya kuangalia ubora wa vyuo binafsi na vya serikali hapa Iraq, chini ya viwango vya ubora.
Rais wa kamati ya kusimamia ubora wa elimu Dokta Alaa Abdulhasan Atwiyya amesema: “Hakika wizara ya elimu inategemea viashiria vya msingi katika kupima ubora wa elimu wa vyuo vikuu vya serikali na binafsi hapa Iraq”.
Marais wa vyuo na wakuu vya vitengo katika vyuo binafsi mbele ya muwakilishi wa idara ya elimu kutoka wizarani, wamejadili vigezo vya shahada ya juu chini ya maazimio ya wizara namba (112) ya mwaka 2020, kuhusu umuhimu wa kiwango bora cha elimu za wanafunzi na wakufunzi kinacho takiwa, pamoja na kujipanga kwa ajili ya msimu wa masomo wa mwaka kesho.
Kumbuka kuwa vyuo vikuu vyote viwili Alkafeel na Al-Ameed tayali vimesha andaa selebasi ya masomo, inayo kidhi vigezo vyote vya ubora wa elimu ya sekula, na vimepiga hatua kubwa katika hilo na wamepata mafanikio mazuri.