Maktaba ya wanawake imetangaza harakati zake wakati wa ziara ya Arubaini

Maoni katika picha
Idara ya maktaba ya wanawake chini ya kitengo cha elimu na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imetangaza kukamilisha maandalizi yote ya huduma itakazo toa katika ziara ya Arubaini, kwa kiwango kikubwa huduma hizo zitatolewa kwa njia ya mtandao kutokana na kuwepo kwa janga la maambukizi ya virusi vya Korona.

Kiongozi wa idara bibi Asmaa Raádu Abadi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kila mwaka tumezowea kufanya harakati mbalimbali wakati wa ziara ya Arubaini, tukiwahudumia mazuwaru wa kike wa kila umri kupitia vituo tofauti vya kutoa huduma, lakini mwaka huu kutokana na mazingira ya afya na kwa ajili ya kuheshimu maelekezo ya idara ya afya, ambayo imepiga marufuku mikusanyiko ya watu, tumeamua kutumia njia ya mtandao na kutoa huduma kupitia jukwaa la (ZOOM Cloud)”.

Akaongeza kuwa: “Mwaka huu tutatoa huduma kupitia intanet, tumeandaa program maalum tutakayo tumia katika siku za ziara, huduma kubwa tutakayo toa ni kufanya kongamano chini ya anuani isemayo: (Na kwake nimeongoka) na kauli mbiu isemayo: (Hussein ni chemchem isiyo kauka na harakati isiyo kufa), kutakua na vikao vya mazungumzo na mashairi kila siku, tutajadili mambo yanayo husu Husseiniyya na faida zake, pamoja na kuangazia huduma zinazo tolewa na mawakibu Husseiniyya”.

Kumbuka kuwa maktaba ya wanawake imezowea kutoa huduma za aina mbalimbali kwa mazuwaru wa Abu Abdillahi Hussein (a.s) kila mwaka, na mwaka huu imelazimika kutoa huduma kwa njia ya intanet kutokana na janga la Korona, bado inaendelea na harakati mbalimbali walizo anza kuzifanya mara tu baada ya kutangazwa janga hilo na wataendelea nazo hata baada ya ziara ya Arubaini, wanahakikisha wanatekeleza jukumu la kuhudumia watu kadri ya uwezo walio nao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: