Waziri wa mambo ya ndani ametembelea Atabatu Abbasiyya tukufu na amekutana na makamo katibu mkuu

Maoni katika picha
Baada ya Adhuhuri ya siku ya Jumanne (11 Safar 1442h) sawa na tarehe (29 Aprili 2020m) waziri wa mambo ya ndani Sayyid Othumani Ghanimi pamoja na Bulgedia jenerali Abdul-Amiir Rashidi Yarallah na kamanda wa polisi wa Karbala Ahmadi Zawini na jopo la viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama wametembelea Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa ajili ya kuangalia maandalizi ya kuwapokea mazuwaru wa Arubaini.

Baada ya kumaliza kufanya ziara katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) wamefanya kikao na makamo katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Mhandisi Abbasi Mussawi Ahmadi na baadhi ya wajumbe wa kamati kuu, wamesikiliza maelezo kwa ufupi kuhusu mkakati wa Atabatu Abbasiyya tukufu, katika kupokea mazuwaru wa bwana wa mashahidi na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) wanaokuja kwenye ziara ya Arubaini ikiwa ni pamoja na kujadili mikakati ya ulinzi na usalama.

Waziri amepongeza ushirikiano mzuri uliopo kati ya Atabatu Abbasiyya na vyombo vya usalama vya mkoa, kwa ajili ya kuhakikisha amani na utulivu kwa mazuwaru pamoja na kuwepo kwa janga la maambukizi ya virusi vya Korona.

Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa mkakati wa ulinzi, utoaji wa huduma na afya, aidha imetangaza utayali wake wa kupokea mazuwaru wa Arubaini.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: