Vituo vya Ashura: Tukituo la mzee na Imamu Zainul-Aabidina (a.s) huko Sham

Maoni katika picha
Wanahistoria wanasema kuwa Yazidi –laana iwe juu yake- aliamuru mateka wa Imamu Hussein (a.s) wasimamishwe mbele ya msikiti, wakasimama hapo ili waangaliwe na watu kama sehemu ya kuwadhalilisha. Mara akatokea mzee mmoja karibu na wanawake wa nyumba ya Hussein (a.s) na familia yake, akasema: Kila sifa njema anastahiki Mwenyezi Mungu aliye kuuweni na akampa nguvu kiongozi wa waumini dhidi yenu.

Sayyid Abdurazaaq Muqarram anasema: Hapo Imamu Sajaad (a.s) akaanza kumuelewesha mzee yule na kumuongoza katika njia ya yaki, hivyo ndio walivyo watu wa nyumba ya Mtume (a.s), wako tayali kumuongoza kila mtu.

Ali bun Hussein (a.s) akamuambia: Ewe mzee unajua kusoma Quráni? Akasema: Ndio. Akasema: Umesoma aya isemayo: (Sema: Sikuombeni malipo yoyote kwenu ila mapenzi katika kujikurubisha)? Yule mzee akasema: Nimeisoma. Akasema (a.s): Sisi ndio jamaa wa karibu ewe Mzee, je umesoma aya isemayo: (NA JUWENI ya kwamba ngawira mnayo ipata basi khums (sehemu moja katika tano) ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume na jamaa..)? Akasema ndio; akasema (a.s): Sisi ndio jamaa tulio tajwa kwenye aya hiyo, je umesoma aya isemayo: (Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu enyi watu wa nyumba ya Mtume na kukusafisheni barabara)? Akasema: nimesoma; akasema (a.s) sisi ndio watu wa nyumba ya Mtume tuliokusudiwa katika aya hiyo ewe mzee.

Yule mzee akakaa kimya kwa muda, akijutia maneno aliyo ongea, akasema: nyie ndio wao?!. Ali bun Hussein (a.s) akasema: Hakiyamungu sisi ndio hao bila shaka, kwa haki ya babu yetu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) sisi ndio hao!. Yule mzee akalia na akatupa kilemba chake, kisha akainua kichwa juu na akasema: Ewe Mola mimi natubu kwako kwa kuwachukia watu hawa, na mimi najitenga na maadui wa Muhammad na Aali Muhammad (s.a.w.w) wa kijini na binaadamu.

Halafu akasema: Je kuna toba?. Akamuambia (a.s): Ndio.. Ukitubu Mwenyezi Mungu atakubali toba yako na utakua bamoja na sisi. Akasema: Mimi natubu, habari ya mzee huyo ikamfikia Yazidi bun Muawiya, akaamuru auwawe na akauwawa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: