Wanahabari wa Atabatu Abbasiyya tukufu wanaripoti matembezi ya wapenzi wa Imamu Husseini (a.s)

Maoni katika picha
Katika mkakati ulio andaliwa na kitengo cha habari katika Atabatu Abbasiyya tukufu kwenye ziara ya Arubaini, ni kuripoti matukio ya matembezi ya wapenzi wa Imamu Hussein (a.s) kuanzia kituo cha mbali kabisa kusini ya Iraq, hadi kwenye kaaba ya msimamo na uhuru mji mtakatifu wa Karbala kupitia nyenzo tofauti.

Kabla ya kuanza kwa harakati za ziara tulifanya vikao “Makamo rais wa kitengo cha habari Ustadh Muhammad Asadi aliuambia mtandao wa kimataifa Alkafeel kuwa, katika vikao hivyo tulijadili mkakati wa utangazaji kulingana na vifaa vilivyopo, na jinsi ya kuripoti tukio hili muhimu la kimataifa, ambalo kila vyombo vya habari vikijitahidi kuripoti bado havilipi haki yake”.

Akaongeza kuwa: Utangazaji wa safari hii utahusisha sekta nyingi, miongoni mwa sekta hizo ni:

  • - Kutengeneza masafa maalum ya kurusha matangazo bure na kwa ubora mkubwa (clean), kuanzia kituo cha mbali kabisa kusini ya Iraq hadi katika kaaba ya msimamo Karbala tukufu, kwa kutumia mitambo ya kisasa chini ya wanahabari walio bobea wanao tumia ujuzi wao wote kuhakikisha wanafikisha sauti ya ziara hii kila sehemu ya dunia.
  • - Kurusha vipande vya uombolezaji kutoka ndani ya malalo mbili takatifu na kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili.
  • - Urushaji wa habari kupitia njia ya kielektronik, ambapo mtandao wa kimataifa Alkafeel unanafasi kubwa katika sekta hiyo, ulianza kurusha matangazo hayo tangu siku za kwanza kabisa za matembezi ya Arubaini kuanzia kituo cha mbali hadi Karbala, wanarusha habari na picha, pamoja na harakati za Atabatu Abbasiyya na huduma wanazo pewa mazuwaru sambamba na maandalizi maalum yanayo yanywa kwa ajili ya kupokea mazuwaru, bila kusahau mambo mbalimbali yanayo ripotiwa na toghuti hiyo kupitia mitandao yake yote ya kielektronik.
  • - Kuandaa ratiba ya kuangazia huduma zinazo tolewa na Atabatu Abbasiyya tukufu pamoja na mambo yenye uhusiano na ziara kiroho.
  • - Kurusha maelekezo kwa mazuwaru.
  • - Kurahisisha utendaji wa waandishi wa habari wa (redio, luninga, magazeti na mitandao), pamoja na kuwapa vitambulisho maalum na kuwatengea sehemu rasmi ya kutekeleza majukumu yao.

Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa mkakati maalum wa kupokea mazuwaru wa Arubaini, unao endana na mazingira ambayo taifa linapitia kwa sasa, na utangazaji ni moja ya sehemu za mkakati huo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: