Zaidi ya maukibu (900) zimetoa huduma kwa mazuwaru wa Arubaini katika mkoa wa Misaan

Maoni katika picha
Kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya katika Ataba mbili tukufu kimesema kuwa: “Mawakibu zilizo shiriki kuwahudumia mazuwaru wa ziara ya Arubaini katika mji wa Misaan zimefika (975) zilizo sajiliwa, bado kuna makumi ya mawakibu na Husseiniyya pamoja na nyumba za watu zilizo toa huduma bila kusajiliwa toka siku ya kwanza, idadi hiyo ni ndani ya eneo la mipaka ya mkoa huo”.

Kwa mujibu wa maelezo ya makamo rais wa kitengo Sayyid Hashim Mussawi, amesema: “Mkoa wa Misaan ni moja ya mikoa inayo pitiwa na makundi makubwa ya watu wanaokwenda kufanya ziara ya Arubaini, maukibu za kutoa huduma zimeenea kwenye barabara zote zinazo tumiwa na mazuwaru, pamoja na kuyapa umuhimu mkubwa maeneo yanayo pitiwa na mazuwaru wengi zaidi”.

Akafafanua kuwa: “Kuna maukibu (496) zitashirikiana na maukibu zingine kutoa huduma katika mkoa wa Karbala na kwenye barabara zinazo ingia kwenye mkoa huo”.

Akaongeza kuwa: “Maukibu hizo hazijaishia kutoa huduma peke yake, bali zimetoa huduma za matibabu pia na kutoa maelekezo ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, sambamba na kushirikiana kwao na vikosi vya ulinzi na usalama, na baada ya kuisha misafara ya mazuwaru katika mkoa huu wahudumu wa mawakibu hizi watakwenda Karbala kufanya ziara na kupata utukufu mara mbili wa kutoa huduma na kufanya ziara”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: