Miongoni mwake yameanza kutoa huduma: Majengo yanayo tumika kutoa huduma kwa mazuwaru chini ya Atabatu Abbasiyya yametangaza utayali wake wa kupokea mazuwaru wa ziara ya Arubaini

Maoni katika picha
Majengo yanayo tumika kuhudumia mazuwaru chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu yaliyopo kwenye barabara zinazo elekea Karbala kupitia njia tatu kuu (Bagdad – Baabil – Najafu) yametangaza kukamilisha maandailizi ya kupokea mazuwaru wa Arubaini ya Imamu Hussein (a.s).

Vitengo vya Atabatu Abbasiyya tukufu vimejipanga kupokea mazuwaru wa Arubaini, ziara ambayo mwaka huu inafanywa kwa namna ya pekee kutokana na kuwepo kwa janga la maambukizi ya virusi vya Korona, kwa hiyo wamefuata masharti yote ya kujikinga na maambukizi ya virusi hivyo kwa mazuwaru na watumishi, chini ya maelekezo ya wizara ya afya na idara ya madaktari wa Atabatu Abbasiyya.

Baadhi ya majengo hayo yamesha anza kutoa huduma, kutokana na mazuwaru kuanza kuwasili mapema mwaka huu, hususan upande wa Baabil ambao kuna jengo la Alqami na upande wa Najafu ambao unamgahawa (mudhifu) wa Ataba wa nje, na maukibu Ummul-Banina ambayo ipo chini ya chuo kikuu cha Al-Ameed. Kuhusu jengo la Shekh Kuleini lililopo upande wa barabara ya Bagdad bado linasubiri mazuwaru wanao tarajiwa kuwasiri hivi karibuni.

Maandalizi hayo hayatofautiani na maandalizi ya muda yanayo fanywa na mawakibu msimu wa ziara kila mwaka na kuja kutoa huduma kwa mazuwaru, kama vile maukibu ya Ushaaqu-Alkafeel iliyopo mkabala na ofisi za tarbiya za mkoa wa Karbala na maukibu ya shamba boy wa Alkafeel iliyopo kwenye barabara inayo pita upande wa Husseiniyya ya Karbala, na maukibu ya jengo la Saqaa/2 pamoja na maukibu ya kiwanda cha Al-Atwaa na ile ya chuo kikuu cha Alkafeel katika mkoa wa Najafu, na maukibu ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya kwenye barabara ya (Yaa Hussein)/ Najafu – Karbala.

Huduma zinazo tolewa ni chakula, vinywaji na huduma za afya na kuongoza walio potea pamoja na huduma za maelekezo ya kielimu na usomaji sahihi wa Quráni, pamoja na huduma zingine nyingi nafasi haitosi kutaja zote.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: