Mazuwaru wa Arubaini wanawasili Karbala na Atabatu Abbasiyya imetangaza kuwa imejiandaa kuwapokea

Maoni katika picha
Siku ya pili mfululizo mazuwaru wa Arubaini wameanza kumiminika kwa wingi katika mji wa Karbala, kufanya ibada ya ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), misafara hiyo unakuja kwa kutembea kwa miguu huku wakipewa huduma ya ulizi, afya na zinginezo.

Mazuwaru wanaoelekea Karbala hivi sasa wanamiminika kutoka mikoa ya kusini (Muthanna na Diwaniyya), pamoja na mikoa ya Misaan na Waasit, hutumia njia tofauti kufika Karbala, baadhi yao huanza kwenda kumzuru kiongozi wa waumini (a.s) katika mkoa wa Najafu, halafu ndio wanaenda Karbala kwa kupitia barabara ya (Najafu – Karbala), na baadhi yao hupitia mkoa wa Baabil kisha wanaingia katika mkoa wa Diwaniyya halafu wanaingia Karbala, na wengine hususan wanaotoka mkoa wa Misaan huenda hadi mkoa wa Waasit kisha hugawika sehemu mbili, baadhi yao hupitia mkoa wa Diwaniyya na wengine mkoa wa Baabil kisha huenda hadi Karbala.

Kuna kundi la mazuwaru walio wasiri kufanya ziara ya mapema, kila mwaka wao huja mapema kwa ajili ya kuwahi kwenda kutoa huduma kwenye mawakibu zao mikoani kwao, hivyo hufanya ziara mapema na kurudi, hali kadhalika wahudumu wengi wa mawakibu hufanya ziara mapema kisha hurudi kwenda kuhudumia mazuwaru, kazi ambayo huisubiri kwa hamu kubwa na muda mrefu, ukizingatia kuwa mwaka huu ni wa pekee kutokana na kuwepo kwa janga la maambukizi ya virusi vya Korona.

Nayo Atabatu Abbasiyya tukufu imetangaza kuwa imejiandaa kupokea wageni wote wa Abu Abdillahi Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), kuanzia kwenye majengo yake ya nje hadi ndani ya haram tukufu, kwa namna ambayo inaendana na ugeni wa mamilioni ya watu wanaotarajiwa kuwasiri ndani ya siku chache zijazo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: