Kitengo kinacho hudumia uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu kimekamilisha maandalizi ya ziara ya Arubaini

Maoni katika picha
Kitengo kinacho simamia uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu kimekamilisha maandalizi ya kuwapokea mazuwaru wa bawana wa mashahidi na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) wanaokuja kwenye ziara ya Arubainiyya, watumishi wake wote wamejiandaa kuhudumia mazuwaru na kuhakikisha wanatembea bila msongamano.

Rais wa kitengo tajwa Sayyid Naafii Mussawi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Watumishi wa kitengo chetu wamekamilisha maandalizi yote ya ziara ya Arubaini, wameweka utaratibu utakao saidia kufanikisha ziara hiyo”.

Akaongeza kuwa: “Mkakati wa kitengo hiki unahusu uimarishaji wa ulinzi na usalama, kwa kuweka askari wanao simamia matembezi ya mazuwaru na kutoa huduma mbalimbali, kama vile kugawa maji na kuandaa sehemu za kuswalia na sehemu za kupita mawakibu na mazuwaru”.

Akaendelea kusema: Watumishi wetu wanaendelea kusafisha kwa kutumia zana tofauti, wanadumisha usafi katika maeneo yote yanayo zunguka Atabatu Abbasiyya ndani ya kipindi chote cha ziara.

Akasema: Aidha tunatoa huduma kwa vyombo vyote vya habari vinavyo penda kurusha matukio ya ziara ya Arubaini kutokea ndani ya uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu.

Kumbuka kuwa kitengo kinacho simamia uwanja wa katikati ya haram mbili chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, ni sawa na vitengo vingine vya Ataba, kimejiandaa kutoa kila aina ya huduma kwa mazuwaru wa Abu Abdillahi Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) katika ziara hii ya Arubainiyya inayo hudhuriwa na mamilioni ya watu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: