Kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya kimesema: Jumla ya maukibu (2382) zimeshiriki kuhudumia mazuwaru wa Arubaini katika mkoa wa Diwaniyya

Maoni katika picha
Mkoa wa Diwaniyya ni moja ya vituo vya misafara ya watu wanaokwenda Karbala kumzuru Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) katika kumbukumbu ya Arubaini, asilimia kubwa wa mazuwaru wa mikoa ya kusini hukutana katika mkoa huo, maukibu za wenyeji wa mkoa huo pamoja na wakazi hutoa huduma kwa kila anaepita kwenye mkoani hapo, mwaka huu jumla ya maukibu (2382) zimeshiriki kutoa huduma kwa mazuwaru, huku maukibu (485) zitaenda kutoa huduma katika mkoa wa Karbala.

Hayo yamesemwa na makamo rais wa kitengo cha maadhimisho ya mawakibu Husseiniyya katika Ataba mbili tukufu Sayyid Hashim Mussawi, akaongeza kuwa: “Idadi hiyo ni maukibu zilizo sajiliwa rasmi na kitengo cha maadhimisho na kupewa vitambulisho vya ushiriki, kuna makumi ya mawakibu na mamia ya Husseiniyya pamoja na nyumba za watu ambazo wamefungua milango na kutoa huduma kwa mazuwaru tangu siku ya kwanza, tena kuanzia mbali kabisa ya mipaka ya mkoa bila kusajiliwa”.

Akafafanua kuwa: “Kuna mawakibu za wakazi wa mkoa huu zimeenda kwenye mikoa mingine kutoa huduma kwa mazuwaru, huku zingine zikishirikiana na maukibu za mikoa mingine kuhudumia wazuwaru katika mkoa wa Karbala na kwenye barabara zinazo elekea Karbala”.

Akabainisha kuwa: “Maukibu hizo hazijaishia kwenye kutoa huduma pekeyake, bali zimetoa ushirikiano mkubwa kwa vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na idara ya afya ya mkoa, baada ya kuisha misafara ya mazuwaru katika mkoa huu, watumishi wa maukibu hizo watatembea hadi Karbala kutafuta utukufu mara mbili, utukufu wa kuhudumia mazuwaru na kufanya ziara”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: