Vituo vya Ashura: Majadiliano ya Imamu Muhammad Baaqir (a.s) na Yazidi mbele ya baba yake Zainul-Aabidina (a.s)

Maoni katika picha
Wanahistoria wanasema kuwa, wakati Imamu Zainul-Aabidina (a.s) alipoingia kwa Yazidi, alikua pamoja na mtoto wake Muhammad Baaqir (a.s) akiwa na miaka miwili na miezi kadhaa, Yazidi alipo muona akasema: Umeona vipi alivyo fanya Mwenyezi Mungu ewe Ali? Akasema: Nimeona hukumu ya Mwenyezi Mungu aliyo pitisha kabla ya kuumba mbingu na ardhi.

Yazidi akaomba ushauri kwa wafuasi wake, wakamshauri amuuwe, na wakasema maneno machafu ambayo hatujayanukuu, Abu Jafari Muhammad (a.s) akashtushwa na mamne hayo, akamsifu Mwenyezi Mungu kisha akasema kumuambia Yazidi: Wamekushauri tofauti na washauri wa Firáun, alipo waomba ushauri kuhusu Mussa na Haruna, hakika wao walimuambia: (Mpe muda yeye na nduguye) na wafuasi wako wamekushauri utuuwe. Yazidi akasema: kwa sababu gani? Akasema: washauri wa Firáun walikua wema, na hawa sio wema, hauwi mitume na watoto wa mitume ispokua mtoto wa haram. Yazidi akakaa kimya.

Kitabu cha maqaatil kimeandika kuwa, Ali bun Hussein (a.s), alipo simama mbele ya Yazidi alisema: Hamtupi chakula na kutunyanyasa na sisi tunawakirimu, hatuwaudhi na nyie mnatuudhi, Mwenyezi Mungu anajua sisi hatuwapendi, wala hatuwalaumu msipo tupenda. Yazidi akasema: Swadakta!. Lakini baba yako na babu yako walitaka kuwa viongozi, namshukuru Mwenyezi Mungu aliye wauwa na kumwaga damu zao.

Kisha Yazidi akasema: Ewe Ali, hakika baba yako alikata kizazi changu na hakutambua haki yangu, aliupinga uongozi wangu, Mwenyezi Mungu akamfanya kama ulivyo ona.

Ali bun Hussein (a.s) akasema: (Hautokei msiba katika ardhi wala katika nafsi zenu ila umekwisha andikwa katika kitabu).

Yazidi akamuambia mtoto wake Khalidi: Mjibu ewe mwanangu!. Khalidi hakupata cha kusema. Yazidi akasema: (Na misiba inayo kusibuni ni kwa sababu ya vitendo vya mikono yenu, naye anasamehe mengi).

Ali (a.s) akasema: Hiyo ni kwa yule aliye dhumumu. Kisha akasema (a.s): (Mwenyezi Mungu huzipokea roho zinapo kufa). Yazidi akanyamaza. Ali bun Hussein (a.s) akasema: Ewe mtoto wa Muawiya na Hindi na Swakhar, Utume na uongozi ulikuwa haki ya wazazi wangu kabla haujazaliwa, babu yangu Ali bun Abu Twalib (a.s) katika vita ya Badri, Uhudi na Ahzaab, alikua mshika bendera wa Mtume (s.a.w.w), na baba yako na babu yako walikuwa washika bendera ya ukafiri.

Ibun Nama Alhilliy anasema: Ali bun Hussein (a.s) anasema: Nikasema nikiwa nimefungwa: Unaniruhusu kuongea? Yazidi akasema: Ongea, na usiseme kwa sauti. Akasema (a.s): Nimesimama kisamamo kisicho mfaa mtu kama mimi, unadhani kitu gani atafanya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) akiniona mimi nimesimama nikiwa nimefungwa namna hii? Akawaamia waliokua pembeni yake. Mfungueni.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: