Kikosi cha Abbasi kinafanya kazi kubwa katika ziara ya Arubaini

Maoni katika picha
Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji kwa kushirikina na vyombo vingine vya ulinzi na usalama, kimeimarisha ulinzi kwenye barabara zote za kuingia Karbala wakati huu wa ziara ya Arubaini, ili kuhakikisha mazuwaru wanafanya ibaza zao kwa amani na usalama.

Makamo kiongozi mkuu wa kikosi cha Abbasi (a.s) Sayyid Haidari Mussawi ameuambia mtandao wa kimataifa Alkafeel kuwa: “Kila mwaka kikosi cha Abbasi hushiriki katika kuimarisha ulinzi kwenye ziara ya Arubainiyya, askari wake huwekwa sehemu tatu kuu, ambazo ni: (Najafu – Karbala/ Baabil – Karbala/ Bagdad – Karbala) pamoja na kwenye mitaa ya ndani ya mji mtukufu wa Karbala”.

Naye muwakilishi wa kikosi hicho bwana Murtadha Fauzi amesema: “Kazi za kikosi hicho hazijaishia kwenye kulinda amani peke yake, bali wanatoa pia huduma zingine pamoja na matibabu, wameweka vituo vya afya katika maeneo tofauti, pamoja na kufanya kazi za kusafisha na kupuliza dawa sehemu wanazo lala mazuwaru, sambamba na huduma ya kubeba mazuwaru pia”.

Kumbuka kuwa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji kila mwaka hushiriki kulinda mazuwaru wa Arubainiyya, na ziara zingine kubwa katika mji wa Karbala.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: