Sayyid Swafi: Umma usiokua na Imamu Hussein (a.s) unaupungufu.

Maoni katika picha
Kufuatia kuanza kwa mradi wa tablighi katika ziara ya Arubaini, unao simamiwa na kuendeshwa na hauza tukufu ya Najafu, kulikua na ujumbe wa Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi ulio gusa nukta nyingi, muhimu katika hizo ni:

 • - Mradi wa tablighi umejikita katika mahitaji ya mazuwaru hasa katika ziara hii tukufu, kwenye sekta ya dini na jamii.
 • - Kutembea kwa miguu kwa bwana wa mashahidi (a.s) kunaonyesha umuhimu.
 • - Mazuwaru wengi hutumia msimu huu kuangalia nafsi zao na kutafakari kwa muda mrefu, pamoja na kutumia muda wa kwenda kwa bwana wa mashahidi (a.s), sambamba na kutaka kupata majibu ya baadhi ya maswali yao, hususan wanapokuwa katika mazingira mazuri kiroho, hupata maswali mengi akilini kwao kutokana na kushughulika sana ndani ya mwaka mzima, yanaweka yakawa sio maswali ya kiibada peke yake, yanaweza kuwa mambo ya kijamii na kidini, kwenye mambo ya muamalaat (vitengo) na katika baadhi ya mambo ya kiitikadi na kimaisha, kama vile uhusiano wa mtu na familia au marafiki, sehemu ya mahitaji yake inaweza kuwa ni kuhusu maswali hayo, hauza ya Najafu imeweka vituo kwenye barabara yote, na ndugu zetu watukufu wamejiandaa kujibu maswali hayo.
 • - Kazi hii inamatokeo mazuri ambayo ni kudumisha uhusiano mzuri baina ya mazuwaru na baadhi ya wanachuoni, kwa sababu kuna baadhi ya maswali yanaweza kuhitaji muda kupatiwa majibu ya kina, au baadhi ya maswali yanakua hayana upande mmoja, upande mmoja upo na mwingine haupo, jambo hilo hubakiza uhusiano mzuri kati ya mwanachuoni na zaairu hata baada ya ziara.
 • - Tumeona athari nzuri katika mradi huu mtukufu kwa miaka mingi.
 • - Hakika msimu wa ziara ya Arubaini ni muhimu sana unafaa kuenziwa historia, na namna ambayo waumini wameendelea kufanya matembezi haya.
 • - Matembezi ya Arubaini yamepigwa vita sana, na watu walikua wanatumia njia mbalimbali ilimradi wafike kumzuru bwana wa mashahidi Imamu Hussein (a.s).
 • - Ziara ya Imamu Hussein (a.s) haizimiki katika nafsi za waumini, na waumini kila mwaka huhuisha ahadi yao kwa bwana wa mashahidi (a.s).
 • - Njia ya kwenda kumzuru Imamu Hussein (a.s) inahuduma zote, miongoni mwa huduma hizo ni tablighi, miaka ya nyuma mambo hayakua hivi, bali ilikua kinyume, kulikua na ugumu mkubwa sana, watu walikua wanafukuzwa na kuzuwiwa kwenda kumzuru Hussein (a.s).
 • - Allah (s.w.t) alikua anaandaa baadhi ya watoto ambao hivi sasa ndio vijana wakubwa, walikua wanaonyeshwa kua hii njia ni hatari, kwa sababu kuna watu wanaozuwia isifuatwe, na kwa upande mwingine wanafundishwa kuwa hii njia ni salama wakiwa bado watoto wenye umri wa miaka mitano, sita hadi kumi, watoto hao walikua wanaongozwa na watu wa familia zao na kusaidiwa jukumu la ziara hadi wafike kwenye lengo lao ambalo ni Imamu Hussein (a.s).
 • - Umma usiokua na Hussein unakua pungufu na umma wenye bwana wa mashahidi Imamu Hussein unakua kamili.
 • - Kila mwaka Imamu Hussein (a.s) huturudisha kwenye mstari wa Imani na uongofu, kila tunapokua na matatizo na dhiki ya nafsi, tunapata utulivu kwa bwana wa mashahidi (a.s), jambo hili sio geni kwani Mtume (s.a.w.w) anasema kuwa: (Hussein ni taa la uongofu), kwa kweli Hussein ni taa la uongofu, taa hili linatuangazia sana.

Akamaliza kwa kusema: “Namuomba Mwenyezi Mungu adumishe baraka za bwana wa mashahidi (a.s) na awalinde mazuwaru watukufu wanaotekeleza kanuni za afya, hakika wanastahiki kulinda nafsi zao na kufanya maadhimisho, tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu aondoe giza katika umma huu, tunahitaji shufaa ya Mwenyezi Mungu kwa utukufu wa bwana wa mashahidi na atupe faraja haraka na watu warudi kwenye maisha yao ya kawaida kwa hasara ndogo, na wala tusione ispokua mambo ya kheri, kila sifa anastahiki Mwenyezi Mungu Mola wa walimwengu na rehma na amani ziwe juu ya Mtume Muhammad na Aali wake watakasifu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: