Mgahawa (Mudhifu) wa Atabatu Abbasiyya tukufu umeanza kutekeleza ratiba ya ziara ya Arubaini

Maoni katika picha
Kitengo cha mgahawa wa Atabatu Abbasiyya tukufu kimeanza kutekeleza ratiba maalum wa ziara ya Arubaini, kwa kufungua madirisha ya nye na kugawa chakula na vinywaji kwa mazuwaru katika milo yote mitatu, sambamba na kuchukua tahadhari zote za afya.

Kuhusu ratiba ya mwaka huu, tumeongea na rais wa kitengo hicho bwana Aadil Hamami, amesema kuwa: “Mwaka huu ratiba yetu inatofautiana na ziara zilizo pita, kwani mwaka huu kuna janga la virusi vya Korona”.

Akaongeza kuwa: “Kabla ya kila kitu tumezingatia kanuni za afya katika kujikinga na maambukizi kwa ajili ya usalama wa mazuwaru, baadhi ya kanuni hizo tulikua nazo hata kabla ya janga hili, kama vile kupuliza dawa, kuvaa barakoa na soksi za mikononi”.

Akaendelea kusema: “Kama ilivyo kawaida ya kitenge hiki (kwenya ziara kubwa) hufungua dirisha za nje zinazo fungamana na mgahawa na dirisha za kibla ya Abulfadhil Abbasi (a.s), pamoja na dirisha lililopo jirani na Ataba karibu na barabara ya Hauraa”.

Akasema: “Tunagawa milo yote mitatu, asubuhi na baada ya adhana ya Adhuhuri, na mlo wa tatu baada ya swala za Magharibaini, katika ugawaji wa chakula tunajali matakwa ya zaairu”.

Akafafanua: “Kazi ya kugawa chakula inafanywa kwa mpangilio mzuri sana, kwa kutumia mistari, kuna mstari wa wanaume na wanawake, kutokana na uzowefu wa muda mrefu walio nao wahudumu wetu, ugawaji huo unafanywa katika mazingira salama zaidi, hawaishii kugawa chakula kwa mazuwaru peke yake, bali wanapewa pia watu wanaojitolea kutoa huduma kwa mazuwaru pamoja na askari”.

Kumbuka kuwa mgahawa wa Abulfadhil Abbasi (a.s), mazuwaru wote wanajua ubora wa huduma zake, huja kuhudumiwa na mgahawa huu kila kwenye tukio (mnasaba) wa Ahlulbait (a.s), hususan kwenye ziara zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu, zikiongozwa na ziara ya Arubainiyya, wahudumu wa mgahawa huu hufanya kazi kwa bidii kubwa katika kutoa huduma.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: